Aidha LHRC wameishauri Serikali kuhakikisha inaongea nguvu katika Utoaji wa elimu ya Utunzaji wa mazingira na uhifadhi wa Vivutio vyetu jambo litakalosaidia kuokoa mazingira na viumbe vyetu ambavyo Tumekuwa tukivipoteza siku Baada ya siku.
Fortunata Ntwele Kutoka LHRC Akieleza machache yaliyowapeleke katika Hifadhi hiyo ambapo amesema kuwa pamoja na kuwa LHRC wanaangalia haki za binadamu lakini mazingira ni swala muhimu sana kwa Binadamu hivyo ni lazima kuyatunza mazingira ili kuwa binadamu imara wenye afya njema. |
Athmani Mmbae ambaye ni afisa utalii wa SAADANI akieleza machache kwa wanahabari baada ya kuwakaribisha wageni kutoka LHRC,ambapo amesema kuwa kutokana na Tangazo la serikali la kuwaruhusu wananchi kuingia Bure kumekuwa na ongezeko kubwa la wananchi wanaokuja kwa makundi kutizama vivutio mbalimbali pamoja na changamoto ya Mvua inayoendelea kote nchini. NAKUPA NAFASI YA KUTIZAMA PICHA MBALIMBALI ZA ZIARA HIYO---- |
No comments:
Post a Comment