Na Zitto Kabwe.
Nimekuwa naulizwa Sana kuhusu uteuzi wa Mwenyekiti wa Chama chetu kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Nimekuwa kimya Kwa sababu tumepokea Taarifa za uteuzi kutoka katika vyombo vya Habari.
Mwenyekiti yuko nje ya nchi na kutokana na tofauti za masaa bado hatujawasiliana nae. Tutatoa tamko kamili atakapokuwa amerejea nchini.
Ninawataka wanachama wote wa Act Wazalendo wawe watulivu na Kama kuna masuala yanayohusu maamuzi ya vikao vya Chama tutawajulisha.
Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto,Mb
Kiongozi wa Chama
No comments:
Post a Comment