MICHEZO

MBWANA SAMATTA ASAINI MKATABA MNONO NA DIAMOND TRUST BANK (DTB)

Diamond trust bank leo juni 18 imesaini mkataba na mwanasoka mashuhuri anayechezea ligi ya kulipwa nchini ubelgiji mbwana samatta.  Makubaliano hayo yamefanyika mapema leo kwenye viwanja vya JM Kikwete Youth Park vilivyopo Kidongo Chekundu jijini Dar es salaam  na kuudhuriwa na watoto zaidi ya 200 toka maeneo mbalimbali ya jiji hilo wenye umri kati ya miaka 6 mpaka 15.

Mchezaji wa timu ya KRC Genk Mbwana Samatta akiongea na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam badaada ya kusaini Mkataba na Diamond Trust Bank kuwa Balozi wa Benki hiyo.
Mbwana Samatta amesaini mkataba wa miezi sita kuwa Balozi benki hiyo na atahusika na shuguli mbalimbali za kiijamii na za kibenki kupitia Nyanja mbalimbali ikiwemo za kidijitali, mtandao na machapisho. Pia katika kuonyesha ubunifu DTB watafanya maojiano na samata live kupitia akaunti yao ya facebook ili wapenzi wa mpira waweze kuuliza maswali na kujibiwa moja kwa moja(mubashara)  na samatta ili kuweza kumfahamu zaidi.

Akiongea na waandishi wa habari mapema leo kwenye makubaliano hayo Samatta aliweza kuipongeza Diamond Trust Benk kwa harakati zake za kuhakikisha mchezo wa kabumbu unasonga mbele. “kwanza niipongeze DTB kwa kudhamini ligi kuu bara na ningependa kuyahimiza mashirika mengine kuiga mfano wa DTB katika kukuza ubora wa mchezo wetu huu tuupendao”Alisema Samatta.
Baadhi ya vijana wakionyesha umahili wao wa kucheza kabumbu mbele ya Mchezaji wa Kimataifa Mbwana Samatta ambaye pia ni Balozi wa Diamond Trust Bank mapema leo jijini Dar es salaam

Mbwana Samatta akionyesha umahili wake mbele ya wadau wa Soka  waliofika viwanjavya JM Kikwete mapema leo jijini Dar es salaam

Mbwana Samatta akiwa kwenye picha ya pamoja na kikosi cha Diamond Trust Bank Kindergaten Team mapema leo jijini Dar es salaam

Mbwana Samatta akiwa kwenye picha ya pamoja na kikosi cha timu ya Diamond Trust Bank

Mbwana Samatta akimkabidhi zawadi mchezaji bora kwa timu ya watoto Nabeel Omary mapema leo jijini Dar es salaam

Mbwana Samatta katikati akiwa na Afsa Masoko Silvester Bahati kulia na Viju Cherian kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa DTB bank
About vicent macha

Post a Comment
Powered by Blogger.