Miss Ubungo mstaafu 2014 Diana Kato leo ameadhimisha siku ya mazingira Duniani kwa kupanda miti na kufanya usafi kwenye shule ya msingi Minazi Mirefu iliyopo kata ya Kipawa manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam.
kwenye shughuli hiyo Diana Kato alimualika Diwani wa kata ya Pugu Ndugu Boniventure Mfuru na waliweze kushirikiana kwa pamoja kuifanya shughuli hiyo. lakini pia waliweza kupewa ushirikiano wa kutosha na Mwalim mkuu msaidizi msaidizi wa shule hiyo Bi. Juliana Msinzo ambaye walikuwa nae mwanzo mpaka mwisho wa shughuli hiyo.
Wanafunzi wa shule ya msingi Minazi Mirefu wakisikiliza kwa makini nasaha wanazopewa na viongozi wa mazingira na faida zake ikiwa leo ni siku ya mazingira duniani |
Mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya msingi Minazi Mirefu Bi. Juliana Msinzo akipanda mti kwenye shule yake akiadhimisha siku ya Mazingira Duniani hii ikiwa ni kulinda na kutunza mazingira. |
Diwani wa kata ya Pugu Ndugu Boniventure Mfuru akipanda mti kwenye shule ya msingi Minazi Mirefu hii ikiwa leo ni maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani |
Miss Ubungo 2014 Diana Kato akimwagilia maji mti weke baada ya kupanda hii ikiwa ni kutunza mazingira kwa kuwa leo ni siku ya mazingira duniani |
Wanafunzi wa shule ya msingi Minazi Mirefu wakishirikiana na Miss Ubungo 2014 Diana Kato kufanya usafi kwenye eneo la shule hiyo leo ikiwa ni siku ya mazingira duniani |
Miss ubungo 2014 Diana Kato akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya msingi Minazi Mirefu Bi. Juliana Msinzo pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo. |
Miss Ubungo 2014 Diana Kato akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule Msingi Minazi Mirefu baada ya kumaliza kufanya usafi kwenye eneo la shule hiyo. |
No comments:
Post a Comment