HABARI ZA KIJAMII

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AWASHA MOTO HOSPITALI YA MWANANYAMARA KUJUA ZAIDI SOMA HUMU

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Salum Hapi leo amepokea misaada ya vifaa Tiba kwa ajili ya hospitali ya Mwananyamara vyenye thamani ya zaidi ya million 400 vilivyotolewa na Jumuiya ya Kiislamu ya Mico pamoja na Makjuice aliyetoa misaada yenye thamani ya milioni moja.
Mkuu wa wilaya kinondoni Mh. Ally Salum Hapi akiongea na wauguzi pamoja na waandishi wa habari kwenye hafla fupi ya kupokea vifaa Tiba vilivyotolewa na jumuiya ya Kiislamu ya mico pamoja na MakJuice leo jijini Dar es salaam
Akiongea na Wauguzi wa hospitali hiyo baada ya kupokea misaada Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mh. Ally Hapi aliongelea swala la baadhi ya watumishi kuwa sio waaminifu kwenye  Hospitali hiyo. Alisema kuwa Swala la misamaha limekuwa ni tatizo kubwa kwenye hospitali ya Mwananyamara milioni 107 ndio fedha pekee za wagonjwa  waliolipia na zaidi million 231 ni misamaaha iliyotolewa kwa wananchi. Ina maana kwamba hospitali inajiendesha kwa hasara kwa kuwa baada ya kupata mapato ya kuongeza vitendea kazi na madawa inalazimika serikali kila siku kutoa pesa ambazo zilitakiwa kufanya mambo mengine na badala yake zinatumika kuongezea manunuzi ya dawa MSD.

Hivyo basi Mkuu wa Wilaya huyo alitoa agizo kwa viongozi wa Hospitali hiyo Mkurugenzi na Mganga mkuu kuweza kumletea taarifa(record) za maandishi za kuanzia tarehe 1 januari mapaka mwezi huu wa 7 zenye nambari za simu za wote waliopatiwa misamaha. Lakini pia Mh. Ally Hapi ili kujiridhisha alihitaji kufahamu mambo yafuatayo kwanza ni watu gani wanapaswa kupatiwa misamaha, njia zipi zinatumika kutoa misamaha, na nani anayetoa maamuzi ya misamaha hiyo.

Jambo lingine ni baadhi ya madaktari kupokea wagonjwa bila kufuata taratibu mgonjwa anapitishwa bila kusajiliwa kwenye daftari au kupatiwa tiba bila kuonyesha vipimo vilifanyika wapi na wengine wanaandikiwa dawa na wauguzi wanamuelekeza kwenye maduka ya nje ya Hospitali ambayo wao wana maslahi nayo hali inayosababisha kupotea kwa pato la hospitali hiyo.Baadhi ya Wauguzi wa Hospitali Mwananyamara wakisikiza hotuba fupi toka kwa viongozi waliowasili kwenye makabidhiano ya vifaa Tiba leo jijini Dar es salaam
Lakini pia swala lingine mkuu wa wilaya alikemea ni kuwepo kwa wafanya biashara nje ya geti kuu la hospitali hali inayosababisha bugza kwa wagonjwa. Hivyo basi ametoa agizo malaka husika ikiwemo polisi kwenda kuwatoa na kuondoa kitoa cha mabasi kilichopo getini hapo ili kuondoa msangamano wa watu wanaofanya biashara eneo la hospitali na kuacha eneo hilo likiwa wazi.

Na mwisho mkuu wa wilaya Mh. Ally Salum Hapi alipongeza Jumuhiya ya Mico Tanzania kwa kutoa misaada hiyo na kuahidi kuendelea kushirikiana na jumuiya hiyo ili kuweza kuapata mambo mengi na mazuri zaidi na kuomba taasisi nyingine kuiga mfano wa jumuiya hiyo kuweza kujitolea kwa wagonjwa mbalimbali. Pia alipenda kumpongeza kijana aliyonyesha moyo wa dhati wa kujitolea kwa wengine Mack Juicy kwa kusaidia vifaa tiba kwa ajili ya afya ya mama na mtoto.

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Salum Hapi akikabidhiwa vifaa Tiba na Rais wa Mico Tanzania Al Haji Marwisu Msii
Mkuu wa wilaya Kinondoni Ally Salum Hapi akipokewa msaada uliyotolewa na Mkurugenzi wa MakJuice Bw. Makoye PhilbertOPD Manager wa Hospitali ya Mwananyamara Bi. Teddy Uled akishukuru kwa niaba ya wauguzi wa Hospitali ya Mwananyamara
picha ya pamoja baada ya makabidhiano ya vifaa Tiba yalifanyika Hospitali ya Mwanayamara jijini Dar es salaam
Baadhi ya Vifaa Tiba viliyotolewa mapema leo Hospitali ya Mwananyamara jijini Dar es salaamAbout vicent macha

Post a Comment
Powered by Blogger.