Ikiwa
ni siku kadhaa kupita Tangu Mkurugenzi wa
kampuni ya VIP Engendering na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL James Rugemalira
na Habinder Seth Sigh, Mwenyekiti mtendaji wa PAP ambao walitajwa katika Kashfa ya Escrow Kufikishwa
mahakamani kwa kesi ya uhujumu uchumi Tanzania kupitia Acount ya Escrow
Hatimaye chama cha siasa cha Allience for democratic Change kimeibuka na
kupongeza Juhudi za Rais Magufuli za kutetea Rasilimali za nchi huku wakiwataka
watanzania kumuacha Rais afanye kazi yake kwani yeye ndiye anayejua anataka
kutupeleka wapi.ANAANDIKA EXAUD MTEI----
Katibu Mkuu wa chama cha ALLIANCE FOR DEMOCRATIC CHANGE ADC Ndugu Doyo Hassan Doyo akiwashukuru watanzania mbalimbali waliofika katika futari hiyo |
Akizungumza
na waumini mbalimbali wa kiislam na watanzania katika Futari maalum
iliyoandaliwa na chama hicho Katika makao makuu yake yaliyoko Jijini Dar es
salaam Katibu mkuu wa chama hicho Doyo hassan Doyo amesema kuwa kitendo cha
Rais Magufuli kuonyesha dhahiri kuuchukia ufisadi na kupambana nao ni kitendo
cha kupongezwa na kila mtanzania na sio cha kubezwa kwani wapo wengi
walioshindwa japo kufikia hapo alipofika kwa sasa.
Naibu katibu mkuu U.P.D.P, Ndugu F,MUKUWA akisalimia baada ya kuwakilisha chama chake katika shughuli hiyo |
Amesema
kuwa watanzania sasa wanastahili kumuombea Rais wao na kumuunga mkono katika
vita hii kubwa na kuacha maneno ya kubeza kwani vita hiyo sio ya Rais mwenyewe
bali ni ya watanzania wote dhidi ya rasilimali za nchi kwa ujumla.
Akizungumzia
sakata hilo la Account ya Escrow ambalo mpaka sasa limeshaondoka na vigogo
wawili waliotajwa katika maazimio ya bunge, amesema kuwa Kama Rais ameanza na
hao hatuna budi kuamini kuwa Rais ana nia njema ya kuwakamata wale wote
waliohusika na sio wakati wa kumpangia Rais nani wa kumkamata kwani wakati
anaanza hakuna aliyempangia kuanza.
“Kuna
watu hasa wapinzani ambao sjui hata wanaongea nini hasa,wapo wanaosema kuwa
Rais aende mbali na hapo yani akamate na wale wengine,mimi nasema hivi hivi Rais
akihama na kuingia katika sakata la Richmond na kuamua kuwakamata wale
waliotajwa niambieni nani atapona hapa mjini,tuache kumpangia kazi,yeye ndiye
anayejua anataka kutufikisha wapi”Amesema Doyo mbele ya wanahabari leo.
Aidha
akielezea uwezo wa Serikali ya Tano katika kutatua changamoto za watanzania
amesema kuwa pamoja na wapinzani kunyimwa fursa za kufanya siasa kinyume na
katiba lakini Sasa Rais Magufuli ameanza kuonyesha kuwa anarudi kwenye mstaari
baada ya kuanza kufuata maazimio mbalimbali yaliyowekwa na watanzania likiwemo
la kuwakamata vigogo wa IPTL walioajwa katika sakata la ESCROW.
Shughuli
hiyo ya futari maalum iliyoandaliwa na ADC imewakutanisha watanzania mbalimbali
wakiwemo wawakilishi wa vyama vya siasa kama F.Mukuwa ambaye ni Naibu katibu
mkuu U.P.D.P, na viongozi mbalimbali ambapo katibu mkuu Doyo amewashukuru sana
kwa kufika na kuwatakia maandalizi mema ya sikukuu ijayo.
No comments:
Post a Comment