BIASHARA

TIB CORPORATE BANK KUADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

TIB Corporate Bank imeadhimisha wiki ya utumishi wa umma.
Katika maadhimisho haya, wiki hii wakurugenzi wa benki wamekua mstari wa mbele katika kuwahudumia wateja ili kupata maoni yao na mrejesho utakaowezesha benki kutoa huduma bora zaidi.

Pia viongozi wa benki wamezungumza na wafanyazi wao kupata maoni yao mbali mbali  na mapendekezo yatakayowezesha kuwa na mazingira mazuri zaidi ya kazi ili kuongeza ufanisi katika utendaji utakaowezesha utoaji wa huduma bora zaidi kwa wateja.

 
Meneja rasilimali watu Irene Ungani-Kyara akizungumza na wafanyakazi wa idara ya uendeshaji na idara ya hazina.
TIB Corporate Bank Ltd (TIB CBL) ni benki ya  biashara inayomilikiwa na Serikali. Benki inatoa huduma zote za kibenki za kibishara kwa  mashirika na taasisi za aina mbalimbali za serikali na  binafsi , pia benki inatoa huduma kwa watu binafsi. Benki ina matawi  6 kwa sasa,  Dar es salaam (3), Mwanza , Arusha na Mbeya.

Benki inatoa huduma mbalimbali  kutokana na mahitaji ya mteja. Baadhi ya  huduma hizo ni pamoja na; akaunti za aina mbalimbali kwa makampuni na watu binafsi, mikopo ya aina mbali mbali ya muda mfupi na wa kati, Dhamana za Kibenki(Guarantees),Uuzaji na ununuaji wa fedha za kigeni, ushauri wa uwezekaji katika hati fungani,ukusanyaji wa fedha na kuwezesha malipo ya jumla kwa makampuni pamoja na ulipaji wa mishahara kwa njia rahisi na ya haraka

Mkurugenzi wa uendeshaji Karoli Shayo akimuelekeza mteja namna ya kujaza fomu za kufanya muamala wa benki katika tawi la Samora. Pamoja nae ni Mkurugenzi wa biashara Mwallu Mwachang’a na meneja rasilimali watu Irene Ungani-Kyara

About vicent macha

Post a Comment
Powered by Blogger.