Guest of honor Lord Mayor of Dar es salaam city Isaya Mwita delivering a speech during a commemorating the UN road safety week today at Upanga Dar es salaam
President of AAT Nizar jivan welcomming the Guest of honr Lord Mayor of Dar es salaam Isaya Mwita and invited Guest to be part of function in innaguration of road signs set near school zone by AAT to save lives of Young children at Shaban Robert Road Upanga today.
Director and CEO of AAT Mr Yusuf Ghor speeking to Invited Guest during the function of the program of installing appropriate road signs near the schools to save the lives of students .
Mayor of Dar es salaam Isaya Mwita during the function of the program
President of AAT Nizar Jivan giving a gift to guest of honor Lord Mayar of Dar es salaam Isaya Mwita to apreciate his support toward the initiative of saving lives of young children and all road users.
Lord Mayor of Dar es salaam city Isaya Mwita innagurating one of road signs set by AAT during the program of installing road signs near the schools Shaban Robert Road Upanga Dar es salaam.
Students from Olympio and Diamond Primary school partcipating in the function of innagulation of the road signs near their schools set by AAT and FIA .
The group photo of pacitpants including Students from Olympio and Diamond Primary school during the function of innagulation of the road signs near their schools set by AAT and FIA .
Miss Tanzania Diana Edward adressing the audience during the function hosts by AAT and FIA to save lives of Young children today.
Some of road users including students given some knowledge of using zebra closing by Mr Kombo as a public relation officer of AAT
NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amewataka madereva wanaowasafirisha wanafunzi wanaosoma shule nilizopo katikati ya jiji kuwashusha na kuwachukua ndani ya kuta za shule badala ya kuwashusha na kuwachukua nje.
Meya Mwita aliyasema hayo jijini hapa leo wakati wa uzinduzi wa wiki ya Kimataifa ya usalama barabarani ,ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa utaratibu wanaoutumia madereva hao ni hatari kwa wanafunzi kwani inawalazimu kuvuka barabara.
Alisisitiza kuwa iwapo watatumia utaratibu wa kushusha wanafunzi ndani ya kuta za shule itasaidia kupunguza hatari kwa wanafunzi ikiwemo kugongwa na gari, pikipiki, kupunguza msongamano wa magari barabarani.
" Jambo ambalo linakwenda kufanyika leo ni muhimu sana, limesaidia kuongeza usalama wa watoto wetu ambao wanasoma kwenye shule hizi zilizopo katikati ya jiji, lakini pia linatoa nafasi kwa walimu kuwa na uhakika wa usalama wa wanafunzi wao, najua wakati mwingine mmekuwa na wasiwasi kuhusu usalama wao.
" Nipende kutoa rai kwa madereva, zingatieni jambo hili , mabasi ya shule yawe yanachukua na kushusha wanafunzi ndani ya kuta za shule , utaratibu ambao mlikuwa mnautumia hivi sasa usitishwe mara moja.
Huko ni kuhatarisha maisha ya wanafunzi , ambao badae wangekuwa madokta , wabunge, marais , ndio ambao tunawategemea , watoto ndio Taifa la kesho, nawaomba sawa , walimu mlisimamie jambo hilo,
Aidha Meya Mwita aliwataka walimu na shule kwa ujumla kutumia kwa umakini vifaa vya usalama barabarani katika mitaala ya shule ili kuwafundishia wanafunzi masuala ya usalama barabarani kwani kutafanya watambue elimu hiyo na hivyo kuleta manufaa kwa Taifa.
Alisisitiza kuwa " elimu hii ikifundishwa vizuri itapunguza ajali za barabarani wakati wa kuvuka lakini pia hata pikipiki zitaendeshwa kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani ,bila kuathiri watumiaji wengine wa barabara.
Hata hivyo Meya Mwita aliwapongeza Automobile Association Of Tanzania (AAT), na Federation International Automobile (FIA) kwa kuchukua jukumu la kupunguza ajali barabarani na kuokoa maisha ya wanafunzi.
AIdha AAT, FIA kwa kushirikiana na kitengo cha Usalama barabarani elimu kwa umma, wamefundisha walimu 1000 kutoka shule 51 za jiji la Dar es Salaam kuhusu matumizi sahihi ya alama za barabarani na matumizi sahihi ya barabara ambapo matarajio yake ni kuwafikia wanafunzi wengizaidi.
Sambamba na hilo , AAT, FIA imeahidi kutoa elimu hiyo kwa kila halmashuri za jiji la Dar es Salaam ambapo jumla ya watu 10 watakuwa wakipatiwa mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment