Saturday, June 3, 2017

RAHCO WATOA TAARIFA JUU YA MAENDELEO YA UJENZI WA RELI YA KISASA YA STANDARD GAUGE.




Kampuni hodhi ya rasilimali za reli nchini RAHCO ambayo inasimamia na kutekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya kisasa ya viwango vya standard gauge imekwisha mpata mkandarasi atayefanya kazi hiyo,na imekwisha kabidhi baadhi ya vitendea kazi kwa wataalamu, lakini kulipa malipo ya  awali (advance payment) ambayo ni nusu ya kiwango cha pesa ya mradi wote.
Mkurugenzi mtendaji wa RAHCO,Bw.Masanja Kadogosa ameyasema hayo alipokuwa ofisini kwake jijini Dar es salaam pindi akiongea na waandishi wa habari na mkandarasi wa ujenzi ambaye ni ubia kati ya YAPI MERKEZI toka uturuki na MOTA –ENGENHARIA na CONSTUCAO AFRICA,S.A ya ureno.
Kaimu mkurugenzi mtendaji wa RAHCO Bw. Masanja Kadogosa akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari jana jiji Dar es salaam
“Serikali kupitia RAHCO imekwisha fanya malipo ya awali (advance payment) kwa mkandarasi kwa mujibu wa mkataba wa ujenzi ili kazi iweze kuanza mara moja,lakini tumeshakabidhi jumla ya magari 8 kwa mshauri mwelekezi anayesimamia mradi .”alisema.
Aidha,mkurugenzi amesema ujenzi huu wa kwanza wa kipande cha kutoka Dar es salaam-morogoro(km 300)kuna hatua mbali mbali zinaendelea kwa kuzingatia makubaliano ya aina ya ujenzi wa mradi ambayo ni sanifu-jenga(design and Build)na muda wa mradi huu kukamilika ni miezi 30 tu,na jumla ya kambi tatu (3) kwajili ya mkandarasi kufanyia kazi zake zinaendelea kujengwa katika maeneo ya ilala-shauri moyo(DSM), SOGA (kibaha) na Ngerengere mkoani MOROGORO.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Masanja Kadogosa akikagua ujenzi wa reli ya standrad gauge eneo la ruvu.
Pia, aliendelea kusema kuwa mradi huu ambao utagharimu dola za marekani,1,215,282.000 sawa na (Tsh1.2 billion) utausisha sehemu 5 toka Dar es salaam mpaka mwanza ambapo sehemu zingine zabuni zake zilishatangazwa na hatua mbali mbali za manunuzi  zinaendelea, ni Morogoro hadi Makutopora (336 km),Makutopola hadi Tabora (294 km),na maeneo mengine ni Tabora hadi Isaka (133 km),Isaka hadi Mwanza (248 km)huku akiwataka wale wote ambao wapo ndani ya hifadhi ya reli na walikwisha wekewa alama ya kubomolewa waondoke mara moja kupisha mradi huo.

Hata hivyo,mradi huu ambao ulizinduliwa na mh.Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania JOHN MAGUFULI mnamo tarehe 12/4/2017 unatarajiwa kutoa fursa za ajira kwa wazawa ambapo 20% ya wataalamu watakuwa watanzania na 80% ya wafanyakazi pia watakuwa ni wazawa.
Wakati huo huo Mkurugenzi wa RAHCO alipata fursa ya kufungua njia ya daraja la ruvu lililoharibika vibaya kufuatia mvua zilizonyesha kwa kipindi kirefu hali iliyopelekea kampuni yake na shirika la reli (TRL) kuifunga njia hiyo mpaka ukarabati ulipokamilika hapo jana.
Ukarabati huo ambao ulifanyika usiku na mchana majaribio yake yatafanyika kwa kupitisha treni ya mizigo na baadae ya abiria pindi mainjinia watakapojiridhisha kuwapo kwa hali ya usalama wa njia hiyo

No comments: