Sunday, June 25, 2017

RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI, ALLY HASSAN MWINYI ASHIRIKI NA WATOTO YATIMA KATIKA FUTARI ILIYOANDALIWA NA AAR INSURANCE

Rais Mstaafu awamu ya pili Mhe. Ally Hassan Mwinyi (Kushoto) akimpa maelekezo ya chakua alichokuwa anakula wakati aliposhiriki hafla fupi ya kufuturisha watoto Yatima wa kituo cha Kigogo iliyoandaliwa na Kampuni ya  Bima ya AAR  jijini Dar es Salaam.
Wageni waalikwa wakipakua futari.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Bima ya AAR wakiwapakulia wageni futari.
Mwenyekiti wa Bodi wa kampuni ya Bima ya AAR, Agnes Batengas akiwangoza watoto kwenda kuchukua futari.
Rais Mstaafu wa Awamu ya pili, Ally Hassan Mwinyi akitoa machache mara baada ya kukaribishwa kutoa nasafa zake.
Mwenyekiti wa Bodi wa kampuni ya Bima ya AAR, Agnes Batengas akitoa shukrani zake za pekee kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ally Hassan Mwinyi mara baada ya kushiriki futari na watoto yatima wa kituo cha kigogo jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko na Mauzo Kampuni ya AAR Insurance Tabia Masoud akiwahudumia chakula watoto Yatima kutoka kituo cha Kigogo katika hafla fupi ya kufuturisha iliyofanyika jijini Dar es salaam.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ally Hassan Mwinyi akitoa shukrani zake za pekee mara baada ya kushiriki futari na watoto yatima wa kituo cha kigogo iliyoandaliwa na kampuni ya Bima ya AAR.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Bima ya AAR, Violeth Mordichai akizungumza wakati wa hafla fupi ya kufuturisha watoto Yatima kutoka kituo cha Kigogo jijini Dar es salaam.
Rais Mstaafu awamu ya pili Mhe. Ally Hassan Mwinyi (Kulia) akimkabidhi wa zawadi na Mwenyekiti wa Bodi wa kampuni ya Bima ya AAR, Agnes Batengas (Kushoto) wakati wa hafla fupi ya kufuturisha watoto yatima kutoka kituo cha Kigogo jijini Dar es salaam jana.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Bima ya AAR wakipiga picha ya pamoja na watoto Yatima mara baada ya kuwakabidhi zawadi katika hafla fupi ya kufuturisha watoto yatima kituo cha kigogo jijini Dar es salaam na kuwapa misaada ya chakula, nguo na viatu kwa ajili ya sikukuu ya Eid El Fitri.
---
Dar es salaam: Kampuni ya Bima ya AAR imefuturisha watoto yatima kutoka kituo cha kigogo Jijini Dar es salaam. Hafla hiyo iliyohudhuriwa na Raisi Mstaafu awamu ya pili Mhe. Ally Hassan Mwinyi, pamoja nawahamasishaji mbali mbali katika jamii wanaigusa jamii kwa namna tofauti tofauti. 

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Raisi Mstaafu hawamu ya pili Mhe. Ally Hassan Mwinyi alishukuru kampuni hiyo kwa hafla hiyo ya pamoja kwa kuweza kufuturu na watoto yatima na kugawa mahitaji mbalimbali ikiwemo nguo, viatu na vyakula.

“Ningependa kuwashukuru kampuni ya AAR kwa futari hii pia kuwapongeza katika kazi mbali mbali mnazofanya katika kusaidia jamii kwa ujumla uhusani kwenye swala la afya. Mwezi huu unatukumbusha kufanya yaliyo mema, kusaidia wasiojiweza, kusamehana na kukumbushana mda wa ibada.” Alisema
Aidha wakati wa hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Violeth Mordichai aliwakabidhi watoto hao mahitaji hayo na kuongeza kuwa, futari hiyo ni sehemu ya mpango wake kusaidia jamii hivyo ni vyema katika kipindi hiki wakafuturu pamoja na watoto hao.

“ sisi kama kampuni ya Bima iliyojikita katika kusaidia jamii kwenye swala la afya tumeona ni jambo jema katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani tukapata chakula cha pamoja na watoto yatima kutoka kituo cha kigogo na kuweza kusaidia kwa kuwapa msaada wa mahitaji madogo yatakayoweza kuwasaidia ,hata kipindi cha sikukuu ya Eid el fitri ” alisema 
Pia aliongeza na kusema kwa wale ambao hawajajiunga na huduma zinazotolewa na Kampuni hio wajiunge ili kupata huduma bora ya afya.

No comments: