Sunday, June 25, 2017

JE WAJUA - MAYAI USAIDIA UKUAJI NA USTAWI WA MTOTO?

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), wamesema kuwa watoto zaidi ya milioni 100 wenye chini ya umri wa miaka mitano wamedumaa (wafupi kwa umri wao) kulingana na utafiti uliofanyika wa miezi sita huko Ecuador.


Lishe duni ni sababu kubwa ya kudumaa, pamoja na maambukizi ya magonjwa wakiwa utotoni. Hata hivyo inadaiwa kuwa mtoto akila yai moja kwa siku liwe la chemshwa au kukaanga, husaidia kumfanya mtoto akue kimo na mwenye afya.

Utafiti uliofanywa na Lora Iannotti akiwa na wenzake katika nchi ya Ecuador, kupitia na watoto umri wa miezi sita hadi tisa, umebaini kuwa mayai yanaweza kusaidia katika kuwakuza kimo na kiafya.
Wengi wao wanaishi katika sehemu zenye kipato cha chini hukutwa na maradhi kama vile kudumaa. Hata hivyo wataalamu wa afya wamekuwa wakitafuta njia za kukabiliana na suala hilo kwa watoto.
Miaka miwili ya kwanza katika maisha ya watoto ni muhimu kuwapatia mayai karibia kila siku ili kusaidia haweza kuondoa hali kudumaa ambayo huleta madhara makubwa.

No comments: