Tuesday, June 13, 2017

SAMSUNG YAANZISHA MAPAMBANO DHIDI YA BIDHAA FEKI

Kampuni ya vifaa vya teknolojia ya Samsung Tanzania imeanzisha mfumo mpya wa uwekaji stika mbili katika bidhaa zao kwajili ya utambuzi wa bidhaa halisi ikiwa ni njia ya kupambana na bidhaa feki hapa nchini.
Meneja bidhaa wa kampuni ya Samsung Tanznia bw. Elias Mushi akiongea na waandishi wa habari ambao hawapo pichani mapema leo makao makuu ya kampuni hiyo.

Akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari katika  makao makuu ya kampuni hiyo Jijini Dar es salaam,Meneja bidhaa Bw.Elias Mushi amesema stika hizo zitasaidia kutambulisha bidhaa halisi ya kampuni hiyo lakini sambamba na njia mojawapo ya kupambana na bidhaa feki kwani bidhaa hizo  zinahatarisha afya za watumiaji na mahitaji ya bidhaa bora na halisi zinaongezeka hivyo wanaendelea kufanya jitihada zaidi katika kukidhi matakwa ya wateja ulimwenguni na Tanzania kwa ujumla.

“Ukizingatia bidhaa feki zina hatarisha afya ya watumiaji,mahitaji ya bidhaa bora na halisi yanaongezeka kwa kasi kila kukicha,Samsung tumeendelea kufanya  jitihada zaidi katika kukidhi matakwa ya wateja wetu ulimwenguni na Tanzania kwa ujumla”alisema
Aidha,Meneja amesema wameongeza alama mpya katika bidhaa zao ambapo stika hizo mbili zitawasaidia wateja kutambua bidhaa feki sokoni,kwani stika moja itakua ni stika msambazaji na ya pili itakua stika inayotambulisha bidhaa halisi ya Samsung.

Meneja wa Pyramid Consumers LTD Kareen Babu akiongea na wanahabari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar es salaam.
Pia, Bw.Mushi aliwatambulisha Tanzania Pyramid Consumers ltd,kuwa ndio wasambazaji wao ambao wameingia nao ubia kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa bidhaa za kisasa za kieletroniki za Samsung ndani ya Tanzania zikiwemo Tv,Friji,viyoyozi,mashine za kufulia na macrowave huku akiahidi kuwa wapo mbioni kutambulisha bidhaa mpya toka kampuni hiyo.
Sambamba na hilo,kampuni ya Samsung Tanzania wamezindua kampeni ya “Nunua ,sajili, Na 
Ushinde “ itayoendeshwa kwa mwezi mmoja nchi nzima ikiwa ni kiunganishi cha kupeleka elimu kwa wateja wao na kupata uzoefu wa kuitambua bidhaa halisi ya kampuni hiyo, kabla ya kuendesha bahati nasibu ambayo washindi watapata bidhaa bora zenye waranti ya miezi 12 kila siku toka samsung kwa muda Wa mwezi mmoja ikiwa watajisajili kupitia namba za bidhaa(serial number) walizonunua kwenda 0798 222333.

No comments: