BURUDANI

Mchezaji wa everton Schneiderlin kujiachia ndani ya bongo

Wiki hii Tanzania imebahatika kupata ugeni mwingine kutoka kwa Mchezaji wa Klabu ya Everton, Morgan Schneiderlin ambaye aliambatana na mke wake ajulikanaye kwa jina la Camille ambao walikuja kwa mapumziko mafupi ya Fungate baada ya kufunga ndoa wiki mbili zilizopita.


Mchezaji huyo ambaye atakuja Tanzania Julai 13 na kikosi cha Everton kitakachokuja nchini kwa ajili ya mchezo wake wa kiarafiki na klabu ya Gor Mahia ameonekana kuvutiwa na hali ya hewa ya Tanzania kwani aliposti video kwenye ukurasa wake wa Instagram iliyoambatanishwa na maneno yaliyosomeka “A bit of fun today with the kids from a school in tanzania 😬⚽️❤#lovefootball #thankyoutanzania”.

Akiwa Tanzania wawili hao walienda hadi Mkoani Arusha kwenye hifadhi ya Serengeti kwenda kujionea wanyama na wakiwa huko walipata nafasi ya kutembelea baadhi ya vijiji vinavyokaliwa na wafugaji kabila la Wamasai ambako alipiga picha akionekana kushika fimbo na mwenye uso wa tabasamu.
Hapa Morgan Schneiderlin akiwa na watoto wa jamii ya wamasai


Klabu ya Everton ikiwa ni moja ya Klabu za EPLzinazodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri ya Sportpesa itakuja Tanzania mwezi ujao Julai 13 na itakuwa na mchezo wa kirafiki na klabu ya Gor Mahia mchezo ambao utachezewa uwanja wa Taifa .

About vicent macha

Post a Comment
Powered by Blogger.