HABARI ZA KIJAMII

Serikali imetakiwa kuwaangalia Wajane kwa Chicho Pevu

Hawa ni Baadhi ya Wanawake Wajane walioshiriki katika hafla ya Futari ya pamoja iliyoandaliwa na Uongozi wa Masjid Ghadir na Chuo cha Imam Swadiq, jana Kigogo-Post Dar es salaam.

Mwenyekiti Msaidizi wa Chama cha Wajne Tanzania Wilaya ya Ubungo Dar es salaam Mh Josephine Chale amemtaka Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Magufuli kuwaangalia Wajane kwa jicho la pili ili aone namnagani anaweza kuwasaidia katika Nyanja ya sheria ambayo itazuia wajane kuonewa kwa kudhulumiwa haki zao

Chale amewaomba Wajane nchini wasijisikie wakiwa, kwani kuwa Mjane haina maana ndio mwisho wa Maisha,kwani  haliya kuwa maisha yanaendelea

Aidha Chale ameushukuru Uongozi wa Msjid Ghadir na Chuo cha Imam Swadiq kuweza kuwaalika Wajane katika futari ya pamoja ili Wajane wajisikie kwamba na wenyewe wanatakiwa katika jamii, ili wasijitenge kama vile kwamba wamefiwa basi ndio maisha yamefika mwisho.


Hayo alisema jana katika halfa ya futari ya pamoja na Wajane,iliyoandaliwa na Uongozi wa Masjid Ghadir na Chuo cha Imam Swadiq Vilivyopo Kigogo Post Dar es salaam.

“Napenda tena kuwashukuru Uongozi wa Masjid Ghadir na Chuo cha Imam Swadiq kwa kutualika sisi wajane, tumepata faraja kubwa sana, kwani na sisi tutaenda kufanya kama wanaofanya wenzetu ili tuwape amani wajane.Tunashukuru sana sana,tunamuomba Mungu awape Moyo wa upendo, awape riziki na awape maisha marefu.”
 
Mtumishi wa Chuo cha Imam Swadiq (a.s) Bi Fatma Mwiru akisilisha mada yake mbele ya Wanawake Wajane waliohudhuria katika hafla ya futari ya pamoja iliyoandaliwa na Uomgozi wa Masjid Ghadir na Chuo cha Imam Swadiq, Kigogo Post Dar es salaam.
Kwa upande wake Mtumishi wa Imam Swadiq Bi.Zaynab Ndete alisema lengo la hafla hii ya Futari ya Pamoja na Wajane, ni Tumewaalika wanawake Wajane kutoka  Wilaya mbalimbali za Mkoa wa Dar es salaam, lengo kubwa ni kuzungumza nao na kuwapatia muongozo wa Kisheria, hususani zinazowahusu wao baada ya kufiwa na waume zao.

“Kwa kweli swala ya Ujane ni swala zito ni swala gumu, kwasababu ni swala linalomuhusu mwanamke, kama tunavyoangalia katika jamii yetu ya Kitanzania wajane wengi wanapokuwa wametoza wame zao, wanakuwa ni watu ambao wanakuwa katika matatizo makubwa sana, miongoni mwa matatizo wanayokumbananayo ni kutengwa au kunyanyapaliwa na familia ya mume ,kunyang’anywa haki zao za msingi, kunyang’anywa mali zao ambazo wameachiwa kama urithi na wame zao” alisema Ndete

“Sisi Uongozi wa Masjid Ghadir na Chuo cha Imam Swadiq tumewaita hapa kwanza kuwasaidia waweze kuzifahamu haki zao, wamama wajane hawatakiwi wawe wanyonge pale wanapoondokewa na wame zao,kuondokewa na mume ni jambo Mwenyezimungu (swt) ameliandika kuwa ni lalazima kwani anaweza kuondoka Mume au Mke” aliongeza Ndete.

“Dini ya Kiislam imesimama kidete juu ya kuwatetea wanawake wajane, kwani ukiwa mjane unahaki ya Kuishi kama wengine,anahaki ya kuwa na mali,unahaki ya kuwa Kiongozi,unahaki ya kuwa Bosi, anahaki kuwana amani na upendo, anahaki ya kuwa Muajiriwa, anahaki ya kuolewa na Mwanaume mwingine,anahaki ya kumiliki” alisisitiza

Hatahivyo Mtumishi Ndete aliwaomba Wanawake wajane wasiwe wanyonge na wasimame kidete kuweza kusimamia malezi ya familia zao kwani jukumu la kuwalea watoto aliokuwachia mumewe iko mikononi mwako.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.