Sunday, June 4, 2017

SHEKH HEMED JALALA AWATAKA WATU WA DINI ZOTE KUPENDANA


Watanzania wametakiwa kuwa ni watu wenye upendo, mshikamano, umoja pamoja na amani bila kuangalia itikadi za kidini ama tofauti za madhehebu. Hayo yamesemwa leo tarehe 4 ya mwezi wa 6 katika semina fupi iliyochuku takribani saa moja na nusu iliyofanyika kwenye msikiti wa Al Ghadir Kigogo Jijini Dar es salaam na kuhuduriwa na viongozi wa dini mbalimbali.

Kiongozi mkuu wa Waislam Shia Ithna Asheriya Sheikh Hemed Jalala akiongea kwa msisitizo kuhusu umoja na msikamano kwa dini zote

Semina hiyo iliyokuwa na lengo la kuenzi mchango mkubwa uliyotolewa na Imam Khomeini (sr) ambaye alikuwa ni kiongozi wa dini ya Kiislam. Akiongea kwenye semina hiyo kiongozi mkuu wa Shia Ithna Asheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala alisema kuwa ifikapo siku kama hii dunia nzima inakukumbuka mchango mkubwa uliyotolewa na kiongozi huyo kwani alikuwa ni mfano wa kuigwa kwa jamii yetu. kwani kiongozi huyu alikuwa ni mtu mwenye upendo kwa dini zote mwenye kujari na kuthamini watu wa lika zote bila kuangalia dini zao.

Aliendelea kusema kuwa sisi sote waislamu kwa wakristo tumeletwa na mungu mmoja hivyo basi hatuna haja ya kuwa na tofauti na hata Mitume wetu Mohamad pamoja na Yesu Kristo wote walikuja kuubiri amani na upendo na hakuna hata mmoja aliyekuja kuubiri vita hivyo basi sisi tuanatakiwa kupendana bila kuangalia dhehebu wala dini zetu. Na ndiyo maana leo kwenye kongamano hili wapo watu wa dini zote Waislamu na Wakristo na madhehebu yote kwa kuwa tupo kwa ajiri ya kuendeleza amani na upendo aliyotuachia mzee wetu. Kwa kuwa yeye alikuwa ni mpenda haki na alikuwa hapendi kuona mtu akionewa sio Muislamu kumuonea Mkristo wala Mkristo kumuonea Muislam alichokuwa akikihitaji ni usawa kwa wote. Na kauli mbiu yake ilikuwa ni kuimiza waislam kushikamana kwa kuwa atakayetaka kuua Uislam hatoangalia dhehebu
Sheikh Mkuu wa mkoa Dar es salaam Alhad Mussa Salim akiongea na wageni waalikwa kwenye semina iliyofanyika mapema leo jijini Dar es salaam
Kingozi wa makanisa ya Ufunuo na uzima Tanzania Nabii Poul Bendera akiongea kwa niaba ya dini ya kikristo mapema leo jijini Dar es salaam
Balozi wa Iran nchini Tanzania Mousa Farhang akiongea kwenye semina hiyo mapema jiji Dar es salaam

Nabii Poul Bendera akipeana mikono na kiongozi wa Shia Sheikh Hemed Jalala 
Wageni waalikwa kwenye kongamono la kidini lililofanyika leo jijini Dar es salaam
Baada ya semina wageni waalikwa waliweza kufuturu hapo hapo Msikitini.

No comments: