HABARI MPYA

WAZIRI KABUDI AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA UNICEF NCHINI


Waziri wa Katiba na  Sheria Mhe. Prof.  Palamagamba Kabudi amemkutana na Mwakilishi mkazi WA Shirika la  Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto duniani-UNICEF bibi  Maniza Zaman ofisini kwake mjini Dodoma. 
Katika kikao hicho viongozi hao mbali na kufahamiana pia wamejadili namna ya kuboresha mahusiano baina ya Wizara na UNICEF .
Katika maongezi hayo Bi. Zaman aliishukuru Wizara na taasisi zake kwa ushirikiano inayowapa UNICEF katika programu mbalimbali inazoshirikiana na Wizara.
UNICEF inatekeleza kwa kushirikiana na Wizara katika maeneo ya usajili wa watoto chini ya miaka mitano na kuwapa vyeti vya kuzaliwa, huduma ya msaada wa kisheria na mkakati wa haki mtoto.


About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.