Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mwasiliano kwa kushirikiana na Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFFA) wana furaha
kuujulisha umma kwamba kwa mara ya
kwanza kabisa Tanzania itakuwa mwenyeji wa Kongamano la Global Logistics Summit 2017.
Kongamano hilo litafanyika kwenye Hoteli
ya Ramada Resort Dar Es Salaam, tarehe 23 hadi 26 Agosti 2017.
Kongamano hili la kiulimwengu litakaribisha
zaidi ya wageni 350 wakiwa mawakala wa kusafirisha mizigo, wajumbe wa
kibiashara, washiriki wa kibiashara, maafisa wa serikali, mabalozi kutoka
ukanda wa Afrika na Mashariki ya Kati, n.k. Zaidi ya nchi 32 toka ulimwengu
mzima zinategemewa kuhudhuria na kushiriki mkutano huu toka dunia nzima.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe.
Prof. Makame Mbarawa ameipongeza TAFFA kwa jitihada zake za kutengeneza ufahamu
ambao ulihitajika kwa muda mrefu katika sekta ya uchukuzi ambayo ni muhimu
katika taifa lolote sababu inawezesha usafirishaji wa watu na mizigo.
“Kuleta kongamano la GLS,
2017 mlangoni mwetu ni mafanikio makubwa na pia fursa nzuri ya biashara zetu
hasa katika kipindi hiki ambacho serikali yetu inahamasisha ongezeko la biashara
na katika bara la Afrika na kwingineko.” alisema Waziri.
Kongamano hili la siku nne
limesifiwa kuwa tukio kubwa la kiuwekezaji katika bara la Afrika ambao litashuhudia
washiriki wote wakuu wakikusanyika.
“Mahusiano miongoni mwa waagizaji, wauzaji,
wasafirishaji, mawakala wa kusafirisha na kutoa mizigo ambao ni wachache kati
ya wengi ili kuleta mabadiliko na kuongeza shughuli za usafirishaji katika ya
sekta ya majini Tanzania, hivyo kuisaidia nchi kupata hadhi yake kama kitovu
cha bandari ki-kanda na hatimaye kukuza uchumi wa Tanzania.”
Kongamano hili pia litaiwezesha Tanzania
kupata fursa ya kukuza uchumi wake kupitia sekta ya usafirishaji na usambazaji
na baadhi ya maswala kama uboreshaji wa bandari na kuifanya iwe ya kisasa,
kuongeza vyanzo vya mapato na changamoto zingine zitapewa kipaumbele kwenye
majadiliano.
Rais wa FIATA, Mr. Stanley
Lim na wageni wengine waandamizi kutoka FIATA na wawakilishi wa nchi mbalimbali
watahudhuria na kuongoza programu ambayo itajielekeza katika kuongelea maswala
ya uchukuzi na biashara katika ukanda wa Afrika na Mashariki ya kati.
Kongamano hili linafanyika
wakati ambao wafanyabiashara wa Kitanzania wanahitaji uelewa zaidi pamoja na
maarifa kuhusu njia bora za utendaji kazi zinazotumika katika dunia hii ya kidijitali
ambapo teknolojia inatawala. Kwa hakika kuna fursa nyingi za ukuzaji wa
biashara Tanzania kwa maana ya usafirisaji na uhifadhi wa mizigo hasa katika
nchi zisizo na bahari kama Burundi, DRC, Rwanda, Zambia, Malawi na Uganda
zinaweza kutumia bandari ya Dar es Salaam kama njia ya usafirishaji mizigo.
“Sisi kama TAFFA tunapiga
hatua kuhakikisha tunaziwezesha biashara kupitia kongamano hili la GLS ambapo
wadau mashuhuri na waliobobea katika fani hizi watatoa maarifa bora kwa wasafirishaji wa kimataifa. Hii ni mara ya kwanza kwa sisi kuwa wenyeji
wa mkutano huu wa kiulimwengu. Tunafurahia sana kupata fursa hii ambayo
itaitangaza Tanzania kama kituo kizuri cha usafirishaji.” Alielezea Ngatunga.
“Hii ni fursa muhimu kwa
taasisi yoyote yenye maslahi na sekta ya usafirishaji iwe kama, wakala, kampuni
ya bima, mtoa huduma, mwanasheria, mtoa bidhaa ama afisa biashara kutengeneza
wigo na mahusiano ya kibiashara. Tunataka kuionyesha dunia kupitia mkutano huu kwamba
Tanzania ni sehemu sahihi kwa biashara za ukanda huu.
Maudhui ya kongamano ni,
“Kuimarisha Usafirishaji kwa ajili ya Uchumi endelevu.”
Kwa sekta ya utalii,
kupitia wavuti ya kongamano http://globallogisticssummit.or.tz/ tumetangaza sehemu nyingi
za vivutio vya Kitalii viliyopo Tanzania. Ni tegemeo letu kwamba wageni
watakuwa na nusu siku ya kutembelea vivutio hivi kwenye siku ya nne na ya
mwisho ya mkutano huu. Washiriki pia wameonyesha nia ya kutaka kutembelea mbuga
ya Serengeti, Selous, Zanzibar na Mlima Kilimanjaro. Hii inaonyesha kwamba
ingawa lengo kuu la mkutano ni sekta ya usafirishaji lakini pia kutakuwa na
faida nyingi zitakazopatikana kwenye sekta ya utalii.
No comments:
Post a Comment