BURUDANI

YOUNG D - KUMALIZA TOFAUTI ZAO NA MZAZI MWENZAKEMZAZI mwenza wa mkali wa Singo ya Bongo Bahati Mbaya, David Genzi `Young D,’ Mamisa amefunguka kuwa amemaliza tofauti zake na jamaa huyo baada ya kukubali kumlea mwanaye ambaye awali alidaiwa kumtelekeza.

Akizungumza na Showbiz XtraMamisa alisema kuwa, wameamua kumaliza tofauti zao wao wenyewe bila kumshirikisha mtu na Young D ameahidi kuwa baba bora kwa mwanaye.
“Namshukuru Mungu kwa sasa nipo sawa na mzazi mwenzangu, tuliyaongea bila kuwekwa kikao na mtu yeyote. Young D amem-chukua mtoto na anaishi na bibi yake (mama wa Young D),” alisema Mamisa.

About vicent macha

Post a Comment
Powered by Blogger.