SIASA

ANGALIA HAPA KUJUA KINACHOENDELEA KWA TUNDU LISSU BAADA YA KULALA RUMANDE

Baada ya kukamatwa siku ya jana mwanasheria mkuu wa chama cha CHADEMA ambaye pia ni mbunge wa Singida mashariki Mh. Tundu Lissu leo wakili wake Bw. Fredrick Kihwelo amaongea na waandishi wa habari kubainisha siku gani atafikishwa mahakamani.

Bw. Fredrick Kihwelo alisema kuwa mpaka sasa wapo kituo cha kati na polisi walimaliza kumuhoji toka jana alipokamatwa na wao wanasubiri kujua hatma yake kama atafikishwa mahakani au vinginevyo kwa kuwa polisi hawakutoa jibu la moja kwa moja.

“Tukiwa kama Mawakili wake lazima tujue kama watampeleka Mahakamani ama la, na kama hawampeleki ni nini kinaendelea wakati ameshahojiwa, leo ni Ijumaa kama asipopelekwa ina maana hadi Jumatatu” alisema Kihwelo

About vicent macha

Post a Comment
Powered by Blogger.