MICHEZO

Mashindano ya Meya CUP yamalizika jana, Sober FC yajinyakulia Kombe.

NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI

MASHINDANO ya Mstahiki Meya wa Jiji  la Dar es Salaam Isaya Mwita ya Ndondo CUP yamemalizika jana ambapo timu ya Sober FC imeibuka  mshindi  na kujinyakulia kombe, jenzi pamoja na mbuzi dhidi ya Soweto FC.

Katika mashidano hayo ambayo yalikuwa na mvuto wa aina yake, yalihudhuriwa na wananchi mbalimbali,viongozi akiwemo  mbunge wa jimbo la Tembeke Abdallah Mtolea, na Madiwani.

Awali mashindano hayo ambayo yalikuwa na ushidani mkali yalihusisha timu 20 ambapo hadi kufikia fainali hapo jana timu mbili za Sober FC na Soweto ndio ziliweza kushiriki hatua hiyo.

Katika mchezo huo ambao ulifanyika katika viwanja vya Mzimuni ,Kata ya Vijibweni ambapo Meya Mwita ni Diwani wa kata hiyo, timu ya Sober ilipata ushindi kupitia kwa mchezaji wao Hassan Gumbo ambae aliipatia timu yake goli la ushindi dakika za lala salama.
Aidha katika mashindano hayo, mshindi wa pili ambaye ni Soweto walijinyakulia zawadi ya jezi pea moja pamoja na mpira huku mshindi wa tatu ambao ni Nondo FC iliibuka na zawadi ya Mbuzi.
Akikabidhi zawadi hizo kwa washindi Meya Mwita ambaye ndio mwaandaji wa mashindano hayo, na Diwani wa kata ya Vijibweni alisema lengo ni kuweka vijana pamoja kwakuwa michezo ni furaha.
Alifafanua kuwa licha ya mashinda hayo yaliyomalizika yalihusisha timu kutoka kata moja ya vijibweni , mashindao yajayo yatahusisha timu kutoka kata mbalimbali ambazo zitapenda kushiriki.
Katika mashindano hayo zawadi nyingine zilizotolewa ni pesa tathilimu shilingi 50,000 ambayo ilitolewa kwa mchezaji bora Ibrahimu Kadabla kutoka timu ya Nondo FC.
Hata hivyo Mbunge wa Temeke  Mtolea alisema kuwa katika mashindano yajayo  timu 13 kutoka jimboni kwake zitashiriki.
 

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.