Monday, July 3, 2017

Meya wa Jiji la DSM Mwita awataka wananch kuwa wa moja bila kujali itikadi ya vyama vyao.


Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita mwenye suti nyeusi akishangilia jambo jana kwenye hafla  ya uchangiaji wa kanisa la TAG lililopo Kivule jijini hapana.


Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza na waumini wa kanisa la TAG jana.

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita katikati Mwenye suti nyeusi akishangilia kwaya iliyomaliza kutumbuiza kwenye hafla hiyo ya uchangiaji wa ujenzi wa kanisa la TAG Kivule jana. Wakwanza mwenye shati jeupe ni Diwani wa kata hiyo Mollel, wapili kushoto ni Mchungaji wa kanisa hilo Amosi Mbiga.

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita katikati mwenye suti nyeusi akizungumza na waumini wa kanisa la Tanzania Assembles Of God jana katika hafla ya uchangiaji wa ujenzi wa kanisa la kisasa lililopo Kivule Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.wapili kushoto Mwenye Shati jeupe na Tai ni Diwani wa kata ya Kivule Mollel, watatu kulia ni Mchungaji wa kanisa hilo Amosi Mbiga. 

.Diwani wa Kata ya Kivule Mollel akizungumza na waumini waliohudhuria hafla hiyo ya uchangiaji wa ujenzi wa kanisa la Tanzania Asemblies Of God jana. katika hafla  hiyo Diwani Mollel aliahidi kuchangia mifuko 25 ya Sementi.

NA CHRISTINA MWAGALA ,OFISI YA MEYA WA JIJI

MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amesema watanzania hawajafikia hatua ya  kubaguana kwa kiitikadi ya vyama, Dini, Kabila badala yake wote wanapaswa kutangaza hali ya Umoja, Upendo na Mshikamano katika nchi yao.

Meya Mwita alitoa kauli hiyo jijini hapa jana, wakati wa harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa Kanisa la kisasa la Tanzania Assemblies Of God  (TAG) lililopo Kivule ,Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini hapa ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa watanzania wanapaswa kuwa wamoja ili nchi iendelee kuwa na amani.

Alisema yapo mambo mbalimbali ambayo yanajitokeza ndani ya nchi ambapo kama watanzania , kwakushirikiana na viongozi wa dini kwa pamaoja  wanapaswa kusimama na kuliombea Taifa ili kuendelea kudumisha amani iliyopo.

" Tangu nimezaliwa sijawahi kushuhudia vita, machafuko katika nchi yetu, kikubwa huwa naona amani iliyotawala, Upendo, na umoja , sasa nawasishi sana ndugu zangu tuendelee kuwa wamoja tusibaguane, kwa namna yoyote ile , ili nchi yetu iendelee kuwa na amani" alisema Meya Mwita.

"Baba wataifa Hayati Mwalim Julius Nyerere enzi ya uhali wake alikuwa akisisitiza sana kulinda amani ya nchi yetu, na sisi ambao tupo hai hadi sasa , mambo ya vyama, Udini, Ukabila tuweke pembeni  tusimame kama Taifa moja.

Awali akijibu risala iliyoandaliwa na uongozi wa kanisa hilo, Meya Mwita aliahidi kuchangia katika ujenzi huo mifuko 100 ya Simenti na kiasi cha Fedha shilingi 500,000 huku aliwataka waumini wa kanisa hilo kujitolea ili kufanikisha  ujenzi huo.

Risala hiyo ilieleza kujenga kanisa la kisasa lenye uwezo wa kuchukua waumini 600 ambapo jumla ya shilingi milioni 95 zinahitajika ili kukamilisha ujenzi huo.

No comments: