Sunday, July 2, 2017

TGNP MTANDAO KUVUMBUA MAZITO KWENYE SEMINA ILIYOFANYIKA TANDIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Wazazi kote nchini wanatakiwa kuwa waangalifu na wapende kuwachunguza watoto wao nyendo zao wawapo majumbani na pia waendapo mashule. Hayo yamesemwa jana kwenye semina iliyofanywa na mtandao wa jinsia Tanzani(TGNP) lengo likiwa ni kuwapa elimu wakazi wa Tandika ili kupinga ukatili wa kijinsia unaofanywa kwenye maeneo yanayowazunguka.
Bw. Speratus Kyruzi toka TGNP Mtandao akiongoza semina iliyofanyika mapema jana Tandika jijini Dar es salaam na kuhudhuliwa na wakazi mbalimbali toka kata za Azimio, Amani na Tandika
Akiongoza semina hiyo Bw. Speratus Kyaruzi aliwaelewesha maana ya ukatili wa kijinsia na kuwaonyesha sinema ya Wanaharakati mbalimbali wakionyesha jitihada zao katika kupinga ukatili dhidi ya watoto wa kike na jamii kwa ujumla na baadhi yao waliweza kutoa shuhuda za mambo mbalimbali waliyoyaona na kuyapitia wao wenyewe.

Baadhi ya wakazi wa Tandika wakiangalia sinema ya kuelimisha ili kujifunza mambo mbalimbali ya ukatili wa kijinsia mapema jana jijini Dar es salaam
Kupitia semina hii imeonyesha kuwa eneo la Tandika linaukatili wa hali ya juu wa kijinsia unaotekelezwa na wanaume wa kata hiyo. Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesema kuwa mapaka leo hii kuna baadhi ya wazazi wakiume wanakataa kuwapeleka watoto wao wa kike shuleni kwa madai ya kuolewa.
Baadhi ya wakazi wa Tandika wakimsikiliza kwa makini muwezeshaji wa semina toka TGNP Mtandao Bw. Speratus Kyruzi kwenye semina iliyofanyika mapema jana jijini Dar es salaam
Akitoa ushuhuda Bi. Khadija Ramadhani alisema kuwa yeye jirani yake aligoma kumpeleka shule ya sekondari mtoto wake wa kike kwa kudai kuwa ameshafikia umri unastahili kuolewa. Na kusema kuwa  mpaka sasa ameshatolewa barua na inasubiliwa ndugu wa pande zote mbili kuelewana kwa pamoja ili aweze kuozeshwa kwa kuwa ameshachezwa ngoma na umri wake unatosha kabisa kuolewa kwa kuwa ameshatimiza miaka  14.

Kulawitiwa kwa watoto wakiume na miongoni mwa matatizo kwenye kata hiyo ya Azimio baadhi ya wakazi wa kata hiyo wakiomba msaada kupitia taasisi na serikali kwa ujumla kuliangali swala hilo kwa umakini zaidi.
Bi. Sharifa Hassani akiongea kwa jazba pindi alipokuwa akitoa maoni yake kwenye semina ya kupinga ukatili wa kijinsia mapema jana jijini Dar es salaam
Bi. Sharifa Hasani ni miongoni mwa waanga wa tatizo hilo kwa kusema kuwa yeye mwenyew mtoto wa kaka yake ambaye alirubuniwa na mbaba mtu mzima ambaye ni mkazi wa Temeke . Huyo jamaa alikuwa akienda kumchukua  shuleni bila walimu na wazazi wake kufahamu na hivyo kuja kugundua ikawa tayari mtoto amelawitiwa kwa muda mrefu ameshaharibika, Na walipojaribu kuulizwa walimu wanasema ana miezi mtoto ajaonekana darasani ndipo kuja kufanya uchunguzi walimgundua mualifu na mpaka sasa yupo chini ya polisi kwa kosa alilolifanya.

Tatizo la ubakaji pia lipo kwa asilimia kubwa kwa mabinti wa eneo hilo, kubakwa mabinti na ndugu zao hata wazazi kubaka watoto wao.

Pili Mkologo yeye alishudia kwa baba aliyemfukuza mkewe na kubaki na watoto wake wakike watatu ambao baadae baba huyo aliamua kuwatumia kama wake zake aliamua kutembea na mwanae mkubwa na bado akaona haitoshi akaamua kutembea na wote mapaka wa mwisho ambae alikuwa ni mdogo sana kwa kuwapa vitisho vya kuwaua endapo watasema yanayoendelea ndani mwao. Na baadae mama kuja kugundua alichokifanya mumewe ikawa muda umeshapita kashawaharibu watoto wote.
Bi. Tatu Khamisi Kitenge akitoa maoni yake kwenye semina ilifayika mapema jana jijini Dar esa salaam
Lakini pia kuna familia ambayo pia wazazi walishindwa kuendesha kwa maadili mazuri na mama alikuwa anapika ugali na kila mtoto anaambiwa akajitafutie mboga. Hali hii ikamfanya binti yao ambae alikuwa anasoma kuweza kushawishiwa na babu yake ambae ni mzazi wa mama yake kwa kumpa pesa za kununulia chipsi, kuku na baadae wazazi walipogundua walimpeleka polisi. Na baadae walimalizana kifamilia na Yule mzee akaachiwa na kuondoka zake pasipojulikana.

Lakini pia tatizo lingine ni katika swala la ugawanaji wa rasilimali bado ni tatizo kwa kuwa kuna mama kwenye kundi hilo waliweza kushirikiana kwa pamoja na mumewe kutafuta mali yeye akiwa anauza vitumbua na mumewe anauza samaki lakini walipogombana mwanamke alikatazwa asiondoke na chochote na vitu vyote vikawa mali ya mwanaume.

Mimba za utotoni vimeshamili kwa kiasi kikubwa na hatimae kuweza kuunda kikundi kinachoitwa "Umoja wa Mama Wadogo" yani umoja huu unawahusisha wale watoto waliozaa wakiwa na umri usiostahili kuzaa ambao ni chini ya miaka 18.
Mdau wa watoto kata ya Amani  bw. Juma Tetele akitoa mchango wake kwenye semina iliyoandaliwa  na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP)  mapema jana jijini Dar es salaam
Na mwisho kabisa mdau wa watoto toka kata ya Amani Bwana Juma Tetele alisema kuwa yeye mpaka sasa ana kesi mbili anazozisimamia za ulawiti wa watoto na kuwaomba wazazi wawe makini na watoto wao wawapo nyumbani na pia waendapo shuleni.  Aliwaomba wazazi ikiwezekana wachukue mawasiliano ya simu kwa walimu ili kupewa taarifa kuhusu maendeleo ya watoto pia wakirudi nyumbani wawena tabia ya kuchunguza walichokifanya shuleni kwa siku hiyo.

Na jambo lingine aliwaomba wazazi kutopendelea kuwaweka vijana wao wadogo na wageni ambao ndugu zao au sio ndugu bila kufahamu tabia zao vizuri, kwani hii inakuwa ni miongoni mwa sabababu za kubakwa au kulawitiwa kwa watoto hao.

Wakazi hao pia waliomba mashirika mengine yanayotetea haki mbalimbali yaweze kuiga mfano wa TGNP wa kuwafuata wananchi na kuwapa elimu na sio kukaa maofisini na kusema tu wao ni wanaharakati." Wanaharakati ni kujitoa kujua wananchi wanachangamoto gani ili kuweza kuwasaidia kuzitatua sio mapaka waje ofisini kwako ndio ujue kuna watu wanashida za kisheria".walisema wakazi hao

Lakini pia wazazi wakike kwa wakiume wametakiwa kukaa na watoto wao wakike kwa wakiume kuwapa elimu ya afya ya uzazi ili kupunguza tatizo la mimba za utotoni na ubakwaji kwa watoto wao wa kike.na ulawiti kwa watoto wa kiume. Na kuwaeleza nini cha kufanya kabla madhara hayo kutokea.

                             
.                            


No comments: