BURUDANI

MUIGIZAJI WA FILAM ZA KIHINDI SANJAY DUTT NDANI YA BONGO

Tanzania imekuwa na neema kubwa sana kwa mawaka huu wa 2017 ya kutembelewa na watu mashuhuri duniani baada ya kuona ujio wa David Backham akiwa na familia yake walipokuja kwa mapumziko.

                
lakini pia tuliweza kuona club kubwa sana huko nchini Uingereza ya Everton iliyokuja kwa mapumziko na kuondoka siku kadhaa zilizopita. timu hiyo iliweka kambi hapa nchini na kucheza mechi na club ya Gor Mahia nchini kenya kwenye uwanja wa Taifa uliopo jijini dar es salaam.

lakini kitu kingine kinachoshangaza baadhi ya wakazi wa nchi hii kuona muigizaji nguri wa filamu za kihindi toka bollwood akionekana kuwepo nchini anaefahamika kwa jina Sanjay Balraj Dutt

Muigizaji huyo amepokelekewa na Mbunge wa Manonga wilaya ya Igunga, Tabora Mh. Seif Khamis Gulamali, na anatarajiwa kutembelea katika mbuga za wanyama za Ngorongoro zilizopo mkoani Arusha.About vicent macha

Post a Comment
Powered by Blogger.