HABARI ZA KIJAMII

TGNP BADO WALIA NA UKATILI WA KIJINSIA.

Wanaharakati kutoka mtandao wa kijinsia wa TGNP waguswa na ukatili wa kijinsia unaofanyika katika jamii na  kuamua kuifanya kuwa agenda kuu kuelekea tamasha la jinsia.
Afisa Program wa Harakati na ujenzi wa pamoja wa TGNP Mtandao Bi. Anna Sangai akitoa mawasilisho kwenye Semina iliyofanyika mapema jana kwenye ofisi za mtandao wa jinsia jijini Dar es salaam
Wakijadiliana jana ndani ya ukumbi wa mtandao huo mabibo jijini Dar es salaam, wanaharakati wamekubaliana kubeba dhana hio ya ukatili wa kijinsia maana wanaamini ukatili unaathiri maeneo mengi yakiwemo ya afya, elimu, jamii na uchumi hali inayopelekea kudidimiza ustawi wa maendeleo kwa mwanamke.
Baadhi ya wanaharakati wakiwa makini kusikiliza Semina iliyofanyika mapema jana ofisi za TGNP Mtandao jijini Dar es salaam
Aidha,Wanaharakati hao wamekubaliana kutumia njia mbali mbali za kisanaa zikiwemo za ushahiri, ngonjera, maigizo na matumizi ya mabango na picha zenye michoro inayoelimisha watu kuhusiana na upingwaji wa ukatili wa kijinsia katika jamii.

Nae, Afisa programu harakati na ujenzi wa pamoja Bi. Anna Sangai amewataka wanaharakati hao kujiandaa vema na tamasha hilo kwani ilo ndilo eneo muhimu la kuonyesha nini mtandao unafanya kwa muda wote lakini pia wanaharakati watumie fursa ya kujifunza  vile vitu ambavyo washiriki wenzao wataonyesha kwani inaweza kuwasaidia hata katika shughuli za uchumi kwani tamasha linalenga kuhusisha watu wa makundi tofauti yakiwemo ya wajasiriamali.
Baadhi ya wanaharakati wakifuatilia Semina iliyofanyika ofisi za Mtandao wa Jinsia(TGNP) Mabibo Dar es salaam
Tamasha la jinsia lenye kauli mbiu ya “Mageuzi ya mifumo kandamizi kwa usawa wa jinsia  na maendeleo endelevu”linatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 5-8 ya mwezi wa 9 mwaka huu katika viwanja vya mtandao mabibo jijini Dar es salaam huku likitarajiwa kuhudhuliwa na wageni mbali mbali kutoka ndani na nje ya nchi.


About vicent macha

Post a Comment
Powered by Blogger.