Monday, July 3, 2017

TGNP MTANDAO WATOA SEMINA YA UKATILI WA KIJINSIA KWA WAKAZI WA MBURAHATI

TGNP Mtandao bado inaendeleza semina zake za kutembelea kata mbalimbali za jiji la Dar es salaam lengo likiwa ni kuwapa elimu wakazi wa kata husika juu ya kupinga ukatili wa kjinsia uliopo kwenye kata zao. Leo ikiwa ni siku ya tarehe 3 julai  wawezeshaji toka TGNP mtandao walitembelea kata ya Mburahati na kuongea na wakazi wa eneo hilo kwenye ukumbi wa Baba Watoto uliopo Mburahati jijini dar es salaam.
Muwezeshaji toka TGNP Mtandao Bi. Agness Lukani akiongoza semina ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyofanyika mapema leo Mburahati jijini Dar es salaamKupitia semina hiyo wakazi wa Mburahati waliongea changamoto mbalimbali zilizopo kwenye kata hiyo ambazo zinatekelezwa kwa makusudi au kwa kuto kujua kwa wafanyao kuwa ni ukatili wa kijinsia na baadhi ya yaliyojadiliwa ni yafuatayo.

Bw. Selemani Shabani akichangia hoja kwenye semina ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyofanyika Mburahati mapema leo jijini Dar es salaam
Mila na Desturi potofu zimekuwa ni miongoni mwa sababu zinazopelekea kuwepo kwa mimba za utotoni kwa kuwa inaeleweka kuna baadhi ya makabila watoto wakifikia umri wa miaka 12 wanapelekwa kwenda kuchezwa ngoma na huko hakuna kinachofundishwa zaidi ya kumjua mwanaume na jinsi ya kumtumia ni siyo mafunzo mema ambayo yatamjenga mtoto huyo kwa maisha ya baadae.
Bi. Amina Omary akichangia mada kwenye semina ya kupinga ukatili wa kijinsia, mapema leo jijini Dar es salaam
Pia imeelezawa kuwa baadhi ya wazazi wa eneo hilo wanashindwa kuyabeba majukumu yao kama wazazi hali  inayosababisha watoto wao kupotea ki maadili. Kutokana nan hili uanakuta mzazi anashindwa kukemea tabia ya mtoto wake kwa kuwa binti huyo huyo akipata pesa toka kwa wanaume wake anampatia na mama anaongezea kwenye pesa ya chakula hali inayofanya mzazi wake wa kike asiwe na sauti kwenye hili.
Bw. Yahaya Konde akichangia hoja kwenye semina iliyofanyika mapema leo jijini Dar es salaam
Na wazazi kuwa wakali kupita kiasi ni miongoni mwa sababu zinazomnyima mtoto haki yake ya msingi hivyo unakuta hata kama mtoto anateswa na mzazi mmoja wapo anashindwa kuongea na mzazi wake kwa sababu ya ukali wake mtoto anakosa mshauri hali inayosababisha mtoto kufuata ushauri wa marafiki au watu wengine wabaya hivyo kuingia kwenye makundi mabaya. Hii imeelezwa kuwa ni sababu ilifanya kuharibika kwa vijana wa eneo hilo.
Bi. Benadetha Mwale akitoa maoni yake kwenye semina ya kupinga ukatili wa kijinsia mapema leo jijini Dar es salaam
Tatizo la kupigwa kwa wamama nalo lipo kwa kiasi kikubwa kutokana na makosa ya watoto wao au ya kwao wenyewe, hii imeelezwa kuwa wamama wengi wanapigwa na kushindwa kutoa taarifa juu ya uonevu uliopo kwa kuogopa kupoteza ndoa zao, hivyo upewa kipigo na asubuhi anatulia na kuendelea na mambo yake bila kujali kuwa anafanyiwa ukatili wa kijinsia.
Bi. Faidha Twalib akichangia mada kwenye semina leo jijini Dar es salaam
Na tatizo la ubakaji lipo kwa asilimia ndogo sana katika maeneo hayo na imeelezwa kuwa mambo hayo  utekelezwa usiku kwa wale mabinti wanaopenda vigodoro na kushindwa kutulia makwao mpaka usiku wa manane wanazunguka kufuata miziki huwa ndio wanapata madhara hayo kwa kuwa kwenye shughuli hizo wanakuwepo watu toka maeneo tofauti tofauti siyo Mburahati peke yake.
Bw. Abdalaah Salehe akitoa maoni yake kwenye semina mapema leo jijini Dar es salaam
Mwisho kabsa walipenda kutoa ushauri kwa serikali kuweza kuwarudisha shuleni wanafunzi wanaopata ujauzito waweze kurudi baada ya kujifungua kwa kuwa hawatafanya mchezo kutokana  watakuwa wamejifunza vya kutosha kwa waliyoyapitia. Hivyo haitakuwa na maana kuwaacha tena mtaani kwani hali hii itawapa mwanya wazazi wa kuwaozesha ingawa umri wao ni mdogo.

Na pia walipenda kuwaelimisha wazazi wenzao wa kata ya Mburahati kujenga tabia ya kukaa chini na kuongea na watoto wao ili kuwafundisha maadili mema na kuwapa elimu ya uzazi ili kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo na jinsi ya kizitatua.
baadhi ya wageni warioudhuria semina hiyo

Pia waliomba kwa TGNP mtandao kuwa na mawakala au vikundi mbalimbali kwenye kila kata ili kuweza kusambaza elimu hii zaidi na watu mbalimbali waweze kupata elimu ili wawaondokane na ukatili huu unaoendelea kwa sasa.

No comments: