TIB Group ina mashirika
matatu yaliyoundwa kimkakati ili kuiwezesha serikali katika kusukuma mbele
gurudumu la maendeleo ya nchi. Mashirika hayo ni
1. TIB Development
Bank Limited
2. TIB Corporate Bank
Limited
3. TIB Rasilimali
Limited
Pamoja na umoja huu,
mashirika haya yanajitegemea kiundeshaji na utendaji, kila moja likisimamiwa na kuongozwa na dira na
dhamira yake chini ya uongozi na bodi zao nazote zikiwa chini ya Wizara ya Fedha
na Mipango.
TIB Group tunakukaribisha kutembelea banda letu la sabasaba ili upate
elimu na taarifa mbali mbali kuhusu huduma zetu.
Taasisi zetu zinatoa huduma
mbalimbali za kifedha ikiwamo
ushauri katika masuala ya mitaji
na uwekezaji, mikopo ya miradi ya kimaendeleo na miundo mbinu pamoja na huduma
mbalimbali za kibenki za biashara.
UWEZO
TUNAO......Tumejipanga
kutoa huduma mbali mbali za kifedha ili kusaidia ukuwaji wa biashara katika
kuwezesha maendeleo ya viwanda.
Mkurugeni mtendaji wa kampuni ya Global Packaging Ndg Joseph Wasonga(wa pili kulia) akiwapa maelezo wakurugenzi wa TIB juu ya bidhaa zinazotengenezwa na kampuni hiyo. Wa kwanza kushoto ndugu Frank Nyabundege Mkurugenzi mkuu wa wa TIB Corporate Bank . Wa pili kushoto Charles Singili –Mkurugenzi Mkuu wa TIB Development Bank na wa mwisho kulia ni Bi Theresia Soka mkuu wa kitengo cha masoko – TIB Corporate Bank Ltd. Kiwanda cha Global Packaging ni miongoni mwa wateja ambao wamenufaika na mikopo inayotolewa na benki ya TIB. Kiwanda hiki ni miongoni mwa viwanda vya kisasa ambavyo vinazalisha vifungashio mbali mbali.
TIB
Development Bank Ltd (TIB DFI) ni Benki ya maendeleo inayojihusisha na
kutoa mikopo mbali mbali ya muda wa kati na muda mrefu. Mikopo hii
inalenga sekta muhimu zinazochochea
maendeleo ya nchi. Sekta hizo ni pamoja na miundo mbinu, uanzishwaji na uundwaji wa
viwanda mbalimbali, miradi ya Gesi, ufuaji wa madini, miradi ya kuongeza
thamani katika mazao ya kilimo na miradi ya huduma za kijamii.
Uzoefu wa benki hii katika
kuwezesha maeneo haya una msingi imara kutoka kuanzishwa kwa Taasisi hii mwaka
1970.
Kwa mawasiliano
zaidi:www.tib.co.tz
![]() |
Wafanyakazi wa TIB Group (TIB Development Bank Ltd, TIB Corporate Bank na TIB Rasilimali Ltd) wakiwa tayari kutoa huduma kwenye viwanja vya Maonyesho - Saba Saba. |
TIB
Corporate Bank Ltd (TIB CBL) ni benki ya
biashara inayomilikiwa na Serikali kwa 100%. Benki inatoa huduma zote za
kibenki za kibishara kwa mashirika na
taasisi za aina mbalimbali za serikali na
binafsi , pia benki inatoa huduma kwa watu binafsi.
Benki ina matawi 6 kwa sasa,
Dar es salaam (3), Mwanza , Arusha na Mbeya.
Benki inatoa huduma
mbalimbali kutokana na mahitaji ya
mteja. Baadhi ya huduma hizo ni pamoja
na; akaunti za aina mbalimbali kwa makampuni na watu binafsi, mikopo ya aina
mbali mbali ya muda mfupi na wa kati, Dhamana za Kibenki(Guarantees),Uuzaji na
ununuaji wa fedha za kigeni, ushauri wa uwezekaji katika hati
fungani,ukusanyaji wa fedha na kuwezesha malipo ya jumla kwa makampuni pamoja
na ulipaji wa mishahara kwa njia rahisi na ya haraka
Huduma zote hizi hutolewa kwa
umahiri na ufanisi mkubwa ili kuhakikisha mteja anafurahia mahusiano yake na
benki. Pia huduma ya ‘Premier Banking’ kwa wale wateja wanaopenda huduma
maalumu na kujitofautisha zaidi. Kwa mawasiliano zaidi:www.tib.co.tz
![]() |
Wafanya kazi wa TIB Corporate Bank Ltd katika picha ya pamoja, wakiwa taya ri kuwahudumia wananchi mbalimbali watakao tembelea banda lao katika maonyesho hayo |
TIB
Rasilimali Ltd ni
taasisi ya tatu katika muundo huu wa TIB Group inayojihusisha na masuala ya uwekezaji
katika masoko ya mitaji kama vile ununuaji na uuzaji wa hisa za makampuni
yaliyoorodheshwa kwenye soko la hisa Dar es salaam (DSE). Pia kutoa ushauri wa
kifedha na kuwezesha utafutaji wa mitaji.
TIB Rasilimali ndio wakala
pekee wa soko la hisa la Dar Es salaam inayomilikiwa na serikali. Imesajiliwa
na mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana(CMSA),pia inajihusisha na masuala ya
usimamizi wa fedha (fund management) chini ya usajili wa Mamlaka ya usimamizi
wa mifuko ya jamii (SSRA).Kwa mawasiliano zaidi:invest@rasilimali.tib.co.tz
No comments:
Post a Comment