Tuesday, August 22, 2017

DAKTARI FEKI WA MUHIMBILI AKAMATWA TENA AMANA HOSPITALI

Daktari feki aliyekamatwa takribani miezi miwili iliyopita katika hospitali ya Muhimbili na kuachiwa bila sababu za msingi kuelezwa kuwa kwanini ameachiliwa?.

Daktari huyo ameibuka tena baada ya kutapeli vijana 8 kwa kudai kuwa yeye ni Daktari kwenye hospitali ya Amana hivyo vijana hao kumuamini na kumpa zaidi ya laki 8 na baadae kuja kushtuka wamesha tapeliwa hivyo kuongea na uongozi na baadae kumkamata mtuhumiwa huyo na mpaka sasa anashikiriwa na jeshi la polisi.

Tukio hilo lililotokea siku ya jana tarehe 21 ya mwezi 8 majira ya saa Tisa mchana na kujaza umati mkubwa wa watu kwenye hospitali hiyo ili kutaka kumuona mtu huyo, Daktari mkuu wa kitengo cha ukimwi kwenye hospitali Bw. Shani Mwaluka anafafanua zaidi tukio hilo.

                                     ANGALIA VIDEO HII KUJUA KILICHOTOKEA....

                     
                              Habari 24 inaendelea kufuatilia na kukujuza kila kinachoendelea.

No comments: