Monday, August 21, 2017

EFM RADIO KUZINDUA TAMASHA LA MUZIKI MNENE NDANI YA TANGA

Kituo chako bora cha matangazo Efm radio kinakuletea tamasha la kila mwaka lijulikanalo kama Muziki Mnene amabalo litazinduliwa rasmi siki ya jumamosi ya tarehe 28/o8/2017 katika mkoa wa Tanga 103.3 fm.
Meneja mkuu wa Efm na Tv E Bw. Denis Busulwa akiongea na waandishi wa habari mapema leo makao makuu ya Efm yaliyopo Kawe jijini Dar es salaam 
Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari Meneja mkuu wa Efm na Tv E Bw. Denis Busulwa alisema tamasha la Muziki Mnene mwaka huu litafanyika kwa muda wa wiki 10 amabao ni sawa na miezi 2 na wiki 2 ambapo muziki utapigwa katika viwanja vya mkoa wa Tanga,Mbeya, Mwanza, Mtwara  na katika Bar mkoa wa Dar es salaam na Pwani.

Muziki Mnene mwaka huu itaenda sanjari nan akampeni ya NJE NDANI ambapo vipindi vinne vitarushwa moja kwa moja katika mtaa husika kwa siku ya ijumaa, na vipindi hivyo ni Joto la asubuhi, Sports headquarters, Uhondo na Ladha 360. Kipindi cha Funga mtaa kitarushwa siku ya jumamosi pamoja na burudani itakayotolewa na RDjs wa Efm na kutakuwa na Jogging asubuhi, Singeli michano kutafuta wasanii wenye vipaji vya muziki wa  singeli, mpira wa miguu kati ya timu ya Efm na Maveteranis/ timu za mkoa katika maeneo husika.

Msemaji mkuu wa Noah Furnishing Bw. Lumumba Farhani akitoa ufafanuzi wa jambo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo makao makuu ya Efm Radio Kawe jijini Dar es salaam 
Tamasha la Muziki Mnene vilevile litaenda sanjari na kampeni ya ugawaji mafuta katika mikoa ya Tanga, Mtwara, Dar es salaam na Pwani, ambapo vyombo vyote vya moto vyenye stika ya masafa ya Efm radio vitapata mfuta bure kama ambavyo zoezi hilo lilivyofanyika katika mikoa ya Mbeya na Mwanza.

Bila kuwasahau wadhamini wa tamasha la Muziki Mnene amabao ni Noah Furnishing pamoja na kampuni ya Biko Tanzania ambapo biko itakuwa ikichezesha bahati nasibu kwenye kila sehemu ambapo Muziki Mnene utakuwepo na mshindi wa kwanza atapata zawadi ya donge nono na wakifuatia na washindi wa papo kwa hapo hadi shilingi milioni moja.
Mkurugenzi wa Masoko wa Biko Tanzania Bw. Goodhope Heaven akitoa ufafanuzi wa jambo fulani katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo jijini Dar es salaam

“Lengo la tamasha hili ni kukutana na kuwashukuru wasikilizaji wetu kwa kuipokea na kushirikiana nasi hadi sasa katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam, Pwani pamoja na mikoa tajwa hapo juu ambayo Efm inasikika , ikiwemo pia kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili katika maeneo yao” alisema Denis Busulwa.
Balozi mpya wa Noah Furnishing Swebe Santana au Rais wa wanaume akiongea na waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika mapema leo Kawe jijini Dar es salaam





No comments: