Monday, August 21, 2017

CCBRT, EFM RADIO NA WADAU MBALIMBALI KUMUUNGA MKONO RC MAKONDA KWA KUTOA MIGUU BANDIA KWA WALEMAVU

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Paul Makonda leo ametangaza kuanza kwa Kampeni ya Uchangiaji wa Miguu Bandia kwaajili ya Wananchi 1,000 wenye uhitaji wa Miguu hiyo ilikuwawezesha kutembea na kufanya shughuli zao.

Katika zoezi hilo Wananchi wataweza kutoa Michango yao kwa njia ya  Simu, Bank au kufika Ofisi za Mkuu wa Mkoa  na kuwasilisha michango yao.

Hatua hii inakuja baada ya wenye uhitaji wa  Miguu Bandia kuwa kubwa tofauti na ile iliyokusudiwa na Mkuu wa Mkoa ya watu 200 ambapo awamu ya kwanza jumla ya watu  650 walichukuliwa vipimo.

Makonda amesema bado uhitaji wa Miguu hiyo ni mkubwa hivyo amewaomba wadau ikiwemo  Makampuni, Taasisi na Watu Binafsi kujitokeze kuchangia ili kutimiza dhamira yake ya kuwafanya walemavu kutembea.

Hadi sasa Wadau mbalimbali ikiwemo CCBRT wamechangia  Miguu 25  kwaajili ya Miguu ya watu wenye Ugomjwa wa Kisukari,Msanii  Mrisho Mpoto  miguu mitatu huku Taasisi za MOI, Ajma Othopedics Medical Service wakiunga mkono zoezi hilo.

Baada ya kuona uhitaji ni mkubwa wa Wananchi Kituo cha Utangazaji cha  EFM na TV E wameamua kumuunga mkono RC Makonda kwa kuibeba Kampeni hiyo kwa kuhamasisha uchangiaji kupitia vipindi mbalimbali.

No comments: