Friday, August 4, 2017

MASAUNI ATEMBELEA KITENGO CHA POLISI CHA KUDHIBITI DAWA ZA KULEVYA,KILWA ROAD JIJINI DAR ES SALAAM.

Naibu Waziri wa   Wizara  ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na watumishi wa Kitengo cha Jeshi la Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati alipofanya ziara katika kitengo hicho kilichopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam, ambapo aliwaagiza kuhakikisha wanapambana na uingizwaji wa dawa hizo kupitia bandari bubu na mianya yote ya uingizwaji na usambazaji. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiongozana na Naibu Kamishna wa Polisi, DCP Mkonyi, wakati alipotembelea  Kitengo cha Jeshi la Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya kilichopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam, ambapo aliwaagiza kuhakikisha wanapambana na uingizwaji wa dawa hizo kupitia bandari bubu na mianya yote ya uingzwaji na usambazaji. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


No comments: