Monday, August 14, 2017

MCT YATOA RIPOTI YA UVAMIZI WA CLOUDS TV

BARAZA la Habari Tanzania (MCT) limezindua Ripoti ya Hali ya Vyombo vya Habari hapa nchini kwa mwaka 2016 (State of the Media Report) ambapo ripoti hiyo hutolewa kila mwaka ili kuushirikisha umma.

Pia Baraza hilo linatoa ripoti kuhusu kuvamiwa kwa Studio za Clouds Media na kubaini jinsi tukio hilo lilivyoathiri uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa uhariri.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Katibu wa Baraza hilo amesema ripoti hiyo haina lengo baya, bali ni kuweka bayana hali ya tasnia ya habari na kwamba hambo hilo si mara ya kwanza kwani baraza hilo limekuwa likitoa ripoti kama hizo kila mwaka.

“Hatujafanya uchunguzi huu kwa kuwa tuna mapenzi na Clouds Media wala kwa sababu tuna mahusiano na Mkuu wa Mkoa, badala yake tumetoa ripoti hii kwa mujibu wa katiba ya MCT,” alisema katibu.

YALIYOJIRI KWENYE RIPOTI HIYO
  • Ripoti imeandaliwa kutoka maeneo mawili ya Tanzania Bara na Visiwani.
  • Methodology: Kusoma machapisho na maandiko pia kuhoji watu mbalimbali.
  • Kuna mahusiano makubwa kati ya mfumo wa kisheria na masuala ya kisiasa. Mfano kupitishwa kwa sheria mbili zinazohusu sekta ya habari.
  • Kinyume na matarajio ya wengi sheria hizi mbili zimeonekana kuwa haziwezi kukidhi nahitaji katika sekta ya habari. Ingawa zilipokelewa kwa Shangwe na wengi lakini matokeo yake ni kuwepo kwa vifingu vinavyominya Uhuru wa habari.

  • Pia zuio la kurushwa kwa matangazo ya Bunge hili pia tumeliangazia katika utafiti wetu. Wananchi wengi wamekiri kuwa usitishwaji huo umewanyima haki ya kujua nini Wawakilishi wao wanafanya ndani ya Bunge.
  • Mwaka 2016 taasisi nyingi za Print Media zilikuwa katika hali mbaya kutokana na matukio mbalimbali ya kufungiwa kwa magazeti.
  • Kupungua kwa matangazo kwenye magazeti hii imepelekea kuathiri sana shughuli za Taasisi hizo.
  • Kushuka kwa usambazaji wa magazeti kutokana na kuingia kwa mitandao ya kijamii pamoja na miundo mbinu.
  • Pia miundombinu ya usambazaji imekuwa mibovu.
  • Kutoka na sheria zisizo rafiki imekuwa pia chanzo cha mauzo ya magazeti kushuka. Pia ukosefu wa teknolojia ya hali ya juu umekuwa ni changamoto.MAFANIKIO
  • Print media zimeendelea sana katika habari za kiutafiti.
  • Redio imeendelea kuwa chombo kinachotegemewa na watu wengi na idadi ya redio pia imeongezeka.ZANZIBAR
  • Kwa Zanzibar kulikuwa na matukio mengi ikiwemo waandishi kunyimwa ushirikiano.
  • Baadhi yao walipewa vitisho na kulazimika kujilinda bila kujali kwamba wanafanya kazi hiyo kwa ajili ya jamii.
  • Hakukuwa na muongozo wowote wa kuwaeleza waandishi kuwa habari hii weka au hii iache.
  • Tumebaini Zanzibar mpaka leo hakuna sheria ya Right to information.
  • Waandishi wengi hawajiendelezi kielimu na baadhi ya waandishi wanafanya kazi bila kuwa na elimu ya kutosha kuhusu taaluma.
  • Zanzibar kuna Vituo vya redio 25 na runinga 22.MAPENDEKEZO
  • Kuna haja ya kutungwa kwa sheria ya Right to information
  • Kuna haja ya specialization kwenye news room
  • Pia traning kwa waandishi hasa kuhusu maslahi yao maana wengi wanajua kutetea maslahi ya jamii lakini ya kwao hawayajui.RIPOTI YA CLOUDS
  • Baraza la habari lilitupa jukumu la kuchunguza kilichotokea kituo cha Clouds Media Group, Machi 17, 2017 ambapo mkuu wa mkoa alienda studio usiku akiwa na askari.
  • Timu yetu ilikuwa na wanachama wanne.
  • Kwa mujibu wa katiba ya habari kifungu cha tatu [E] ndicho tulichokisimamia katika uchunguzi wetu.Hadidu za rejea zilizotumika.
    1. Kwanza kuchunguza kilichotokea
    2. Kubaini askari walioambatana na mkuu wa mkoa
    3. Kutoa mapendekezo kutokana na uchunguzi
    4. Kuandika ripoti
    5. Kuwasilisha kwa wananchi.

  • Timu ilitembelea ofisi za Clouds na kuongea na baadhi ya wafanyakazi, ilifanya mahojiano na wafanyakazi wa TRA, Ilifanya mahojiano maafisa wa haki za bianadamu.
  • Juhudi za timu kuonana na mkuu wa mkoa hazikuzaa matunda yoyote.
  • Tulipitia sheria kuona kama kuna sheria yoyote inayomruhusu mkuu wa mkoa kufanya hicho alichokifanya.

    TULICHOBAINI
  • Tarehe 17/3 mkuu wa mkoa wa Dsm akiwa na askari alienda kwenye kituo cha Clouds usiku lakini afisa wa ulinzi alisema mkuu wa mkoa huwa anaenda mara kwa mara na alishazoeleka.
  • Sio vibaya kwa vyombo vya habari kushirikiana na wanasiasa lakini Urafiki uliojengwa kati ya mkuu wa mkoa na Clouds ndio uliopelekea akawa na ujasiri wa kuingia ofisi kwa namna ile.
  • TCRA ilisema haina wajibu wa kumuadhibu mtu aliyekikosea kituo cha habari kwahiyo yunaona iwepo sheria itakayoruhusu TCRA kuweza kufanya hivyo.
Shuhudia RC Usajili wa Uzaz.

No comments: