Thursday, September 14, 2017

TGNP MTANDAO NA WANAHARAKATI WAKIJADILI CHANGAMOTO ZILIZOTOKEA WAKATI WA TAMASHA LA JINSIA 2017

Baada ya kumalizika kwa Tamsha la Jinsia lililodumu kwa siku 4 mfululizo kuanzia tarehe 5 mpaka 8 ya mwezi septemba katika viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Mabibo jijini Dar es salaam.
Afisa Program na nguvu za Pamoja Bi. Anna Sangai akitoa ufafanuzi wa jambo fulani katika Semina ya GDSS mapema jana jijin dar es salaam
Washiriki wa semina za jinsia maarufu kama GDSS zinazofanyika kila jumatano pamoja na wafanyakazi wa mtandao huo wamekutana kwa pamoja wakiwa na lengo la kujadili mapungufu au changamoto zilizotokea wakati wa Tamasha.

Akiongoza semina hiyo Afisa Program na nguvu za pamoja Bi Anna Sangai alisema kuwa wakati wa tamasha yalitokea mambo mengi kuna mazuri ambayo tunapaswa kupongezwa na kuna mapungufu ambayo yanahitajika kurekebishwa ili yasitokee tena tamasha lijalo.
Bi. Neema Mwinyi akitoa maoni yake kuhusu mapungufu yaliyotokea kwenye Tamasha la mwaka huu mapema jana jijijni Dar es salaam
Na pungufu la kwanza ni kwa upande wa maegesho ya magari (parking) hayakuwa mazuri kutokana kwamba hakukupangwa sehemu maalumu ya magari kwa mfano gari ya mgeni ilitakuwa kuwe na sehemu iliyandaliwa kwa ajiri ya kukaa na wafanyakazi wa TGNP pamoja na wageni waalikwa kulitakiwa kuwe na maeneo ya kukaa gari zao.

Ya pili ni kwamba Mgeni Rasmi Mama Samia Suluhu Hassan hakutembelea mabanda ya wajasiliamali alitembelea mabanda yaliyopo mwanzoni ambayo yalikuwa ya taasisi kubwa kama LHRC, TAMWA, KIVULINI nk.  Lakini katika mabanda ya mbele ambayo yaliandaa vitu vizuri hakufika hivyo hajajua wajasiriamali wamekuja na nini mwaka huu.
Bw. Innocent Siliyo akichangia mada katika mapungufu ya tamasha la jinsia 2017
Kwa usiku wa mwafrika ulipendeza lakini watu hawakufuata utaratibu waliambiwa vazi la siku hiyo ni vitenge, cha ajabu kila mtu alivaa anachokijua yeye hali ilyofanya kuwa siyo tena usiku wa mwafrika wenye vazi maalum, na kingine watoa kuponi siku hiyo walikuwa wakitoa kwa upendeleo hali iliyofanya baadhi ya wageni kukosa kuponi.

Na changamoto nyingine ni kukosekana kwa banda hata moja la kupima afya kama Angaza, Maria stopes nk. Hali iliyowafanya watu  wengi kuulizia mahalali pa kupimia afya zao.
Baadhi ya wanaharakati walioshiriki semina ya GDSS iliyofanyika mapema jana makao makuu ya Mtandao wa Jinsia yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam
Kwa upande wa wana GDSS hawakuchangamkia fursa walipewa banda lakini halikuwa na kazi nyingi za mikono za kushawishi wageni, hali iliyofanya wageni kutoka mikoani kufanya vizuri katika Tamasha la mwaka huu na pia kutofahamu majukumu yao waliyopangiwa na kufanya majukumu ya watu wengine.

Utaratibu haukuwa mzuri kwenye upande wa ugawaji wa chakula kwani haikuwepo sehemu kwa wazee na watu wenye Ulemavu hali iliyowafanya kupanga foleni kama watu wengine, lakini pia kwa wagawa chakula ilikuwa ukimwambia namchukulia mzee au mlemavu wanakataa na kumtaka aende kuchukua mwenyewe.

Na changamoto ya mwisho ni ufungaji wa tamasha watu wengi walikuwa hawaamini kama kweli limefungwa kwani siyo kama kama siku liliyofunguliwa ilikuwa gafla sana, hivyo wadau wanaomba hata usiku wa mwafrika ungekuwa mwisho ili kuchangamsha ufungaji wa tamasha hilo. 

No comments: