Benki ya Exim Tanzania imethibitisha kujitolea kuimarisha ushirikishwaji
wa wananchi kwenye mfumo rasmi wa kifedha nchini kwa kuzindua tawi jipya katika
mkoa wa Dodoma, Tanzania. Utanuzi huu utaongeza uwepo wa Benki ya Exim kuwa na
jumla ya matawi 33 nchini kote.
Akizungumza
katika uzinduzi rasmi Fredrick Kanga, Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu
katika Benki ya Exim Tanzania, alisema, "Utanuzi wa benki ni sehemu ya
mkakati wetu wa kukuza huduma zetu katika
maeneo ambayo yanatuleta karibu na wateja wetu. Tawi litatoa huduma kamili za kibenki
kama vile kuhifadhi pesa, huduma za uwekezaji, na suluhisho za malipo ya
kampuni."
Tawi
la Dodoma, lililopo ndani ya Chuo Kikuu cha Dodoma, litawahudumia wateja wa
Chuo Kikuu hiko, ambacho kina wanafunzi zaidi ya 25,000, wafanyakazi 2000 na
Wizara za Serikali zaidi ya 8 ambazo zimehamia huko. Tawi litawatumikia wateja
wa Jiji la Dodoma pia, kwa kuwa tawi lina umbali wa dakika 5 hadi 7 kwa mwendo
wa gari kutoka katikati ya jiji.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma, Mheshimiwa Jordan Rugimbana alipongeza Benki ya Exim
Tanzania kwa kujitolea kwake "Tunafurahi kuwa na uwepo wa Benki ya Exim
katika mji mkuu wa Tanzania, ili kuimarisha ushirikishwaji wa wananchi kwenye
mfumo rasmi wa kifedha unaowawezesha kupata huduma, bidhaa za kifedha, na mitaji kwa jamii na watu binafsi wa Dodoma.
"
Benki ya Exim ilitambuliwa kama
benki bora kwa huduma ya wateja binafsi mwaka
huu na taasisi ya The Banker ya Afrika Mashariki
na sasa inasherehekea miaka 20 ya mafanikio, ukuaji na kuwa kiongozi katika kuingia
katika masoko mapya barani Afrika. Benki ya Exim ni benki ya Tanzania
inayomilikiwa na faragha ambayo ina uwepo katika nchi 4 na ni benki ya kwanza
ya kimataifa ya Tanzania.
Tangu kukaribisha wateja wetu wa kwanza katika Tawi
la Samora, Dar es Salaam, mwaka wa 1997, Benki ya Exim imeendelea kutanua uwezo
wake kufikia taifa na kanda.
Benki ya Exim katika miaka imeongezeka kwa ujasiri ili kukuza msingi wa
mali na kufanikiwa kutanua uwezo wetu. Shughuli za Benki zinapatikana katika
mikoa ya Dar es Salaam, Zanzibar, Tanga, Morogoro, Kilimanjaro, Arusha,
Manyara, Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Iringa, Mbeya na Mtwara ndani ya Tanzania
na kampuni tanzu nje ya nchi katika Visiwa vya Anjouan, Moheli na Moroni vya
Union of Comoros , kwenye Jamhuri ya Djibouti na Uganda - uwepo wa benki ya
Exim ni wa kimataifa usiofanana na benki nyingine za Tanzania.
Ubunifu ni ahadi tunayowapa wateja wetu. Benki imepata mafanikio makubwa
kwenye uvumbuzi wa teknolojia yenye kwango cha dunia na bidhaa zinazolenga
wateja. Tunajivunia kuwa benki ya kwanza nchini Tanzania kuanzisha kadi za
Mikopo, Hati fungani za kubadilisha biashara, na Taasisi ya mafunzo ndani ya
benki iliyothibitishwa na ISO. Sisi pia tulitoa ufumbuzi wa vituo rununu vya kutolea fedha (ATM), Huduma
ya maasaa 24 kila siku katika matawi kadhaa yenye kuweka hela na mpango wa
kipekee wa fedha kwa wanawake nchini Tanzania. Benki ya Exim ni benki
inayongezeka kwa haraka yenye ubunifu wa kidigitali ambayo ina bidhaa nyingi na
huduma za kuvutia zaidi zilizozinduliwa mwaka 2017 kama kadi zaa benki za
kusafiri, Kadi ya benki ya mshahara kabla ya kulipwa, Kadi ya benki ya dola za
Kimarekani na huduma za benki kwenye simu.
Mwaka jana benki ya Exim ili
pata faida kabla ya kodi ya kiasi cha shilingi 83.3 bilioni ikiiweka benki hiyo
kwenye nafasi ya nne kwa mtaji nchini Tanzania. Katika kipindi cha miaka 20 ya kuwepo
sokoni benki hiyo imejenga taasisi imara kijiografia, katika bidhaa za kivumbuzi,
mahusiano mazuri na wateja na uwezo wake wakutoa huduma kwa haraka zaidi.
No comments:
Post a Comment