Mtaalamu akifafanua katika Mkutano huo |
Wadau wa mazingira katika jiji la Daresalaam wamesifu jitihada zinazofanywa na Kampuni ya OSWAMS za kuhakikisha wanatoa huduma ya kuchakata maji machafu kulekule yanakozalishwa, kwani kufanya hivyo kuna faida kubwa ikiwamo kuyatumia maji hayo kwa matumizi ya kuinua uchumi wa wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa kuitambulisha OSWAMS kwa wadau wa mazingira mkoa wa Daresalaam,Mratibu wa mazingira kanda ya Mashariki (NEMC) Bw. Jafar Chemgege amesema kampuni hiyo imekuja wakati muafaka kwani katika jiji la Daresalaam kwani ni kweli tuna tatizo la majitaka.
Awali, akizungumza na wadau wa mazingira, Eng Mohammed Nassor Juma amesema kampuni hiyo imeweza kutekeleza miradi mbalimbali na kwamba wako tayari kuwatembeza wadau hao ili kubaini ufanisi wa kampuni hiyo kupitia miradi yake iliyofanywa.
Eng Mohammed amesema moja ya wateja wake wakubwa ni Bakhresa Group ambao nao wameridhishwa na uchakataji maji uliofanyika kupitia teknolojia zetu, na kwamba wana uhakika teknolojia inayotolewa na Kampuni yake itasaidia sana katika katika mashule, zahanati na hata watu binafsi.
"Tunauwezo mkubwa wa kufanya kazi ya kuyabadiri maji machafu kuwa maji safi...tuna timu kubwa na tayari tumeajiri zaidi ya watu 50, tunazani kwa nguvu kazi hii tunaweza kwenda mbali na kukidhi mahitaji ya wateja wetu." Alisema
No comments:
Post a Comment