Sunday, October 22, 2017

Famous Furniture,Wasambazaji wa Magodoro ya Sealy Posturepedic na Masofa ya La-Z-Boy Wafungua Duka Dar es salaam

FAMOUS Funiture waelezea malengo makubwa waliyonayo
katika kukua kwa uchumi wa viwanda, ambapo wamewataka 
watanzania kutumia bidhaa bora  za La- Z-Boy ambazo
uboresha zaidi muonekanao wa nyumbani.
Hayo yalisemwa na Meneja wa duka hilo Nabeel Dharser ambaye ni meneja wa duka la thamani za nyumbani wakati wa uzinduzi wa duka hilo oktoba 18 mwaka huu
Mliman City jijini Dar es Salaam.

Nabeel alisema kuwa Famous Furniture Limited iliyosajiliwa na namba 135127 iliona umetambulisha bidhaa bora za nyumbani ilikukidhi soko linalokuwa nchini hapa.
        
"Binadamu hutumia muda mwingi wakiwa wamekaa chini,hii
ndio sababu ya wabunifu,watafiti na wataalamu wa afya kuumiza vichwa kutoa bidhaa zitakazoleta starehe,"alisema Nabeel.

Nabeel alisema mbali na uzinduzi wa huo, duka hilo wanatarajia kufungu maduka mengine 5 maeneo mengine Tanzania.
         
Aidha meneja huyo  alisema kuwa Ryan Beattile kutoka Bravo Group ambao ni wasambazaji wa La-Z-Boy kutoka Famous Furniture wa meeleza starehe ya mkao sio katika muonekano tu bali inakupa  starehe ya mwili na mfumo bora wa egemezi,hasa kama unakaa
kwa muda mrefu.



No comments: