Tuesday, October 24, 2017

IJUE NDOTO KUBWA KULIKO ZOTE KWA NIKK WA PILI

Mwanamuzi kutoka kampuni ya Weusi 'Nikk wa pili' ambaye pia ni msomi mwenye PhD yake mfukoni, amefunguka ndoto yake ambayo amedai ni kuja kuwa rais wa Tanzania
       Tokeo la picha la nick wa pili
Mkali huyo wa singo 'kihasara' amesema sababu ya kutaka kuja kuwa rais ni kubadili baadhi ya mambo kama elimu na uchumi huku akidai kwamba nafasi hiyo ya urais ndio itamuwezesha kufanya hivyo

"Kiuongozi mimi ndoto yangu nataka kuja kuwa rais hiyo ndio kitu ambayo nimewahi ku imagine so sijui hiyo ndoto itakuja kuwa kweli au vipi. Yeah rais wa Tanzania kwasababu mambo ambayo mimi nataka kuja kuyabadilisha nafikiri hiyo position mimi ndio itaniruhusu kubadilisha vitu ambavyo nataka kubadili" amesema nikk wa pili kupitia XXL ya Clouds Fm

Nikk wa pili ameendelea kueleza na kusema kwamba

"Nina vitu vingi vya kubadili kuanzia uchumi, elimu na dira nzima ya maendeleo lakini siwezi kubadilisha nikiwa mbunge au waziri unless nikiwa president hakuna kitu ambacho kinashindikana kikwazo labda ni kwamba mimi sijaamua kuingia kwenye hiyo njia" alieleza

No comments: