Tuesday, October 24, 2017

Hofu yatanda ukosefu wa tiketi mechi ya watani

Mashabiki wa Simba na Yanga wana hofu kubwa ya kuukosa mchezo kati yao utakaopigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Uhuru.
Tokeo la picha la SIMBA NA YANGA
Hofu ya kuukosa mchezo huo unatokana na idadi ndogo ya watazamaji 23,000 tu watakaoingia kwenye Uwanja wa Uhuru wakati ilizoeleka watu 60,000 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kiiingilio ni Sh 10,000 kwa mzunguko na 20,000 kwa jukwaa kubwa. Lakini inaonekana mapema lazima kutakuwa na suala la ulanguzi.

Inawezekana kabisa wako watakaonunua tiketi mapema na kuanza kuziuaza kwa bei kubwa.

Lakini kama zitakatwa getini siku ya mechi, pia inaweza kusababisha vurugu kwa kuwa watu hawatakuwa na uhakika na inawezekana idadi kubwa ikakosa hivyo kusababisha tafrani.

Watu wengi waliochangia kwenye mtandao wa SALEHJEMBE wanaonekana kuwa na hofu ya kukosa tiketi na wanahofia ulanguzi.

No comments: