Thursday, October 12, 2017

KAMPUNI YA UBER YATOA OFA YA AISKRIMU KWA WASAFIRI WAKE JIJINI DAR ES SALAAM



ber icecream.JPG

 Dar es Salaam, Tarehe Oktoba 12, 2017…. Leo kampuni ya Uber nchini Tanzania imewazawadia ‘Aiskrimu’ wasafiri wanaotumia mfumo Uber, hii ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya kuwatuza wasafiri wa Uber. Asikrimu hii itatolewa kwa wasafiri wa Uber watakaobahatika kuchaguliwa jijini Dar es Salaam kati ya saa 6 mchana na saa 9 alasiri.
Akizungumzia kampeni hiyo, Meneja Msimamizi wa Uber nchini Tanzania, Bw. Alfred Msemo amesema, “Katika kampuni ya Uber tunajituma kwa kila hali kutafuta mbinu bunifu na shirikishi zitakazowapa nafasi wasafiri na madereva wetu kufurahia huduma za Uber – isitoshe wao ni nguzo muhimu katika dhamira yetu ya kutoa usafiri salama na wa kutegemewa. Kuanzia saa 6 mchana na saa 9 alasiri leo, wasafiri wa Uber watatumia simu kujishindia Aiskrimu itakayoletwa hadi majumbani au ofisini mwao.”
Ili msafiri aweze kushinda katika ofa hii ya aiskrimu anatakiwa kufungua tu programu ya Uber kati ya saa 6 mchana na saa 9 alasiri, kisha aguse kibendera cha UberIcecream kilicho chini ya skrini ya simu yake na aweke agizo la kuletewa aiskrimu. Ikiwa atabahatika kushinda, gari la Uber litamletea zawadi ya aiskrimu mpaka mahali alipo.
“Ingawa tungependa kuona wasafiri wengi wakishinda aiskrimu katika kampeni hii, aiskrimu itatolewa kwa wasafiri watakaowahi kushiriki katika ofa. Ni wasafiri watakaojishindia zawadi hii pekee ndio watakaoletwa aiskrimu yao” ameongeza Bw. Msemo.

Kampeni hii ya uhamasisho ni mwendelezo wa kampeni ambazo Uber imefanya katika masoko yake ya Afrika Mashariki. Mapema mwaka huu Uber ilikuwa na ofa ya UberChoma nchini Kenya na Uganda, liyoshuhudia wasafiri wa Uber Jijini Nairobi, Mombasa, na Kampala wakiletewa Nyama Choma bila malipo yoyote. Wiki hii wasafiri walipata fursa ya kufurahia chapati maarufu kama Rolex nchini Uganda wakati wa sherehe za Kuadhimisha Siku ya Uhuru nchini Uganda. Mapema mwaka huu wasafiri Jijini Dar es Salaam walipata fursa ya kujishindia pizza kupitia kampeni maarufu iliyojulikana kama UberPizza. “Kwa kweli mojawapo ya sifa za Uber ni utayari wetu wa kuwaalika wasafiri wetu kujiunga na sisi katika kusherehekea mafanikio yetu katika miji mbalimbali. Kampeni ya UberIcecream ni moja kati ya njia nyingi za kuwafikia wasafiri na madereva wetu nchini Tanzania.” Amesema Bw. Msemo

No comments: