Thursday, October 12, 2017

WANAHARAKATI WA GDSS WAMEJADILI MAMBO HAYA KATIKA KILELE CHA SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI

Ikiwa siku ya jana tarehe 11 ya mwezi octoba ni kilele cha siku ya mtoto wa kike duniani TGNP mtandao kwa kushirikiana na wanaharakati wa semina za GDSS wamekutana kwa pamoja kujadili changamoto na utatuzi wa mambo mengi anayokutana nayo mtoto wa kike.
Muwezeshaji wa semina kutoka Camfed Bi. Lilian Walter akiongoza semina ya siku ya mtoto wa kike duniani iliyofanyika mapema jana makao makuu ya Mtandao wa Jinsia TGNP.
Akiongoza semina hiyo muwezeshaji kutoka Camfed Bi. Lilian Walter alisema kuwa kuna mila na desturi nyingi potofu zinazomkandamiza mtoto wa kike na kumfanya aonekane hana haki katika jamii na hii ikiwa ni katika maeneo kama  ya elimu, afya, umiliki wa ardhi na maeneo mengine mengi.

Ikiwa Takwimu zinaonyesha kwa Tanzania kwa wasichana wa umri wa kati ya miaka 10 na 19 ni asilimia 18 ya watanzania wote, ripoti ya maendeleo ya serikali kwa mwaka 2016 inaonyesha udahili  wa wasichana katika shule ya msingi ulizidi wa wavulana kwa asilimia 0.1 lakini wa wavulana kwa sekondari ulizidi wa wasichana kwa asilimia zaidi ya 6.1 hii inaonyesha tunahitaji nguvu ya ziada katika kupinga hali hii.
Dada Nantaka Maufi akielezea namna anavyoilewa siku ya mtoto wa kike duniani na nini wanantakiwa kufanyiwa watoto hawa, ikiiwa ni kilele cha siku ya mtoto wa kike Duniani
Vyanzo vingine vinaonyesha kuwa zaidi ya wasicha 550,000 walikatishwa masomo baada ya kuapata ujauzito na hii ni kwa muongo mmoja uliopita, lakini pia takwimu za (TDHS-MIS) kwa mwaka 2010 zinaonyesha asilimia 27 ya wakina mama wote waliojifungua walikuwa ni wasichana chini ya miaka 20.

Lakini pia imeelezwa kuwa kwa mabinti kukosa elimu ya kujitambua hii inachangia kwa kiasi kikubwa kwa mabinti kupata mimba mapema kwa kurubuniwa na vijana kama boda boda na hata baadhi ya walimu wanaotumia vibaya nafasi zao kwa kuhitaji rushwa za ngono ili kuwapasisha wanafunzi ama kuwapunguzia adhabu watendapo makosa.
Ndugu Innocent Siliyo akichangia mada katika semina ya GDSS mapema wiki hii na mada kuu ikiwa ni siku ya mtoto wa kike Duniani. 
Na jambo lingine ni wazazi pamoja na walimu kutowapa watoto hawa wakike elimu ya afya ya uzazi pia ni tatizo kwani wanashindwa kujiongoza wenyewe na kusababisha watoto hawa kupotea kwa kushindwa kujielewa pindi wanapotongozwa na wanaume, na kutokana bado ni wadogo udanganywa kwa urahisi lakini kama awali wangepatiwa elimu hii ingewasaidia kujilinda na mambo haya.

Wanaharakati hao waliendelea kwa kusema kuwa kwa wazazi kuwa na mambo mengi hata kukosa muda wa kukaa na mabinti zao pia hii inachangia kukuwaharibu watoto na kusisitiza kutowaamini madada wakazi kwa asilimia zote kwani na wao baadhi utekeleza vitendo vya ukatili kwa watoto hao.
Bi. Neofita Kunambi akitoa ushuhuda wa harakati alizopitia kusaidia watoto wakike katika semina ya GDSS mada kuu ikiwa ni siku ya mtoto wa kike Duniani.
Na ili kuondokana na matatizo yote hayo imeelezwa kuwa ni vyema kwa serikali kuweka sharia madhubuti za kumlinda mtoto wa kike na kuhakikisha anapata haki zake za msingi kama elimu, kumiliki ardhi kama ilivyo kwa watoto wakiume, kutoozeshwa kabla ya umri stahiki na kuchukua hatua kali kwa wale wanaokiuka haki za mtoto wa kike.

Wanaharakati kutakiwa kutokaa kimya na kuyafumbia macho mambo mbalimbali yanayosababisha uharibifu kwa watoto hawa ili kupunguza tatizo la mimba na ndoa za utotoni na vitendo vya ukatili dhidi yao hata kama vinatekelezwa na wazazi wao.
Baadhi ya washiriki wa semina ya gdss wakifuatilia kwa umakini semina hiyo.

Lakini pia wanaharakati kuendelea kutoa elimu ya kumlinda mtoto wa kike kwa wanajamii pale kwenye mikusanyiko mbalimbali kama vikoba, mikutano ya mitaa na kujaribu kukaa na vijana kama waendesha boda boda kuwapa elimu hii pia ili wajue kuwa siyo kitu kizuri kutembea na watoto wadogo hii itasaidia kupunguza mimba za utotoni.


                              

No comments: