Ikiwa leo ni
siku ya maadhimisho ya kupinga adhabu ya kifo duniani kituo cha sharia na haki
za binadamu LHRC kikiungana na mtandao wa kupinga adhabu ya kifo duniani kuadhimisha
maadhimisho ya 15 ya kupinga adhabu hiyo.
Akiongea na
waandishi wa habari mapema leo jijini dar es salaam kaimu mkurugenzi wa kituo
hicho Bi. Anna Henga alisema kituo chao kitaendelea kupinga adhabu hiyo mpaka
itakapoondolewa katika sharia ya Tanzania hii ikiwa ni kulinda na kuheshimu
haki za binadamu ikiwemo haki ya msingi ya kuishi.
Anna Henga
aliendelea kwa kusema adhabu ya kifo ni adahabu ya kikatili inayokinzana na
misingi utu na haki za binadamu hivyo haifai kuwepo kwa nchi kama Tanzania
ambayo imeingia na kusaini mikataba ya kimataifa na ya kikanda ya kutetea na
kulinda na kuheshimu haki za binadamu.
Ingawa
inafahamika kuwa adhabu ya kifo utolewa kwa makosa kama kuua kwa kukusudia,
makosa ya uhaini pamoja na ugaidi, na hili siyo kwa mikataba ya kimataifa pekee
bali hata katiba ya nchi ibala ya 14 inalinda uhuru na haki ya kuishi.
Kaimu
mkurugenzi huyo aliendelea kwa kusema kuwa kwa mujibu wa ripoti ya haki za
binadamu ya mwaka 2015 ilionyesha kuwa watu 472 walihukumiwa adhabu hiyo ya
kunyongwa na kati ya hao 452 ni wananume na 20 pekee ni wanawake, na kati ya
hao 228 wanasubiri kunyongwa na 244 wanasubiri rufaa za ingawa adhabu hiyo
haijatekelezwa toka mwaka 1994 japo kuwa mahakama inaendelea kutoa adhabu hiyo.
Lakini pia
imeonekana kuwa adhabu hii inawakumba sana wale watu masikini wasioweza kuwa na
uwakilishi wa kisheria na wanyonge na pia ni vigumu pia kuthibitisha kweli huyu
aliyeshikwa ni mtuhumiwa kweli aliyetenda kosa ni vigumu kupata ushahidi wa
moja kwa moja.
Na jambo
lingine adhabu hii haimpi nafasi mtuhumiwa ya kujirekebisha na badala yake
inakuwa ni ya kulipiza kisasi na hakuna ushahidi wowote wa kuthibitisha kama
kupitia adhabu hii kuna watu wamejifunza na badala yake mauaji yanazidi
kuendelea.
Baada ya
hayo yote serikali imetakiwa kuyafanya yafuatayo ikiwa ni mapendekezo ya kituo
hicho.
Serikali inatakiwa
kurekebisha kanuni ya adhabu ya sharia ya ugaidi yenye kutoa adhabu ya kifo kwa
kosa la mauaji, uhaini na ugaidi.
Serikali kuwaelimisha
wananchi kuhusu kuheshimu haki za binadamu hususani haki ya kuishi na kuweka
mazingira ya uheshimuji wa haki hiyo.
Serikali kubadilisha
adhabu ya kifo na kuweka adhabu mbadala kwa wafungwa waliopo magerezani sasa
kama kuwapa adhabu ya muda mrefu gerezani nk.
Kwa kuwa
imeonekana adhabu hii imekuwa ikimkera rais basi yeye anatakiwa kuwa kinara wa
kuitisha mkutano wa kuiondoa adhabu hii ili yeye na majaji waondokane na mzigo
huu mkubwa wa kutwaa roho za watu.
No comments:
Post a Comment