MWITA : WAIMBAJI WA JIMBO ZA DINI HUBIRINI AMANI
MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amesema waimbaji wa nyimbo mbalimbali za injili, Wanakwaya wanapaswa kutangaza amani na upendo katika Taifa kupitia unjilishaji ili amani iliyopo isiharibiwe na watu wachache.
Meya Mwita amesema kuwa waimbaji mbalimbali ikiwemo kwaya za makanisa wanayonafasi kubwa ya kuhubiri upendo na hivyo nchi ikaendelea kuwa na amani na hivyo kusababisha watu kufanya kaTanzania ikaendelea kusifiwa nakuwa mfano mzuri wa kuigwa.
Meya Mwita ametoa kauli hiyo jijini hapa leo wakati alipokuwa akiendesha harambee ya kuchangia kwaya ya Bikira Maria Mama wa Mungu katika kigango Cha Vijibweni Parokia ya Kigamboni jumla ya shilingi milioni Nne zilipatikana.
Amesema katika kuhubiri amani, Taifa linategemea waimbaji wa jimbo za dini, viongozi wa kiroho makanisani,mikitini na kwamba kwa kufanya hivyo taifa litaendelea kusimama imara pasipokuwa na machafuko yoyote licha ya changamoto mbalimbali zilizopo.
Ameongeza kuwa mbali na kujenga amani lakini pia itawezesha kurudisha maadili kwa vijana, makundi mengine kwakuwa ndio wanaotegemewa katika kutangaza maadili mema katika Nyanja mbalimbali katika jamii.
“Mnapoona viongozi tunafanya mambo yasiyo mpendeza mungu hamna budi kutukemea kupitia njia hii ya unjilishaji kwasababu ujumbe unatufikia” amesema Meya Mwita.
“ Lakini kama mtakuwa mnaona halafu mkanyamaza, itakuwa hamja wasaidia waumini wetu, wananchi ambao wananunua na kusikiliza nyimbo zenu, kila mmoja anajukumu la kuhubiri na kulinda amani ya nchi yake” ameongeza.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa Kwaya hiyo Faustine Kabaganya amemshukuru Meya Mwita kwa na kusema kuwa wanatambua mchango wake kwa kuwa ni kiongozi ambaye anajali makundi yote.
Ameeleza kuwa kwaya hiyo natarajia kuingia studio kwa ajili ya kurekodi albamu na kwamba wamemshukuru kwa mchango ,hamasa ambayo ameitoa katika harambee hiyo.
NA CHRISTINA MWAGALA,OFISI YA MEYA WA JIJI DAR
No comments:
Post a Comment