TGNP Mtandao
ni miongoni mwa mashirika makongwe yaliyokuwa yakipigania vuguvugu la ukombozi
wa wanawake, na kwa kuliona hilo serikali ya Tanzania ikatoa agizo kwa kila halmashauri
kutenga asilimia 5 wa ajili ya wanawake na asilimia 5 nyingine kwa ajiri ya
vijana.
Hayo
yamesemwa mapema jana na muwezeshaji wa semina ya jinsia na maendeleo bi. Bertha
s.masagasi ambae ni afisa maendeleo wa jamii wa manispaa ya ilala alipokuwa
akitoa elimu kwa wanaharakati mbalimbali kuhusu mfuko wa WYDF unaopatikana
katika kila halmashauri hapa nchini.
Muwezeshaji huyo
alisema kuwa mfuko huu ulianzishwa mnamo mwaka 1993 wa uwezeshaji wanawake na
vijana na ulianza utekelezaji wake mwaka huo huo kwa mikoani mingine, lakini
kwa halmashauri za jiji la Dar es salaam zilianza kutenga fedha hizo ikiwa ni
utekelezaji wa agizo hilo mwaka wa fedha 1998/99.
Lakini pia
kwa Tanzania inaonyesha kuwa tumepiga hatua zaidi kwa swala la uwezeshaji na
mpaka sasa kuna mifuko 19 na iliyopo katika serikali za mitaa yetu ni mitatu.
Kundi la
kwanza ni la vijana ambalo mfuko wake upo chini ya wizara ya kazi na maendeleo
ya vijana, na kundi la pili ni la wanawake ambalo msimamizi wake ni Wizara ya Afya
Jinsia Maendeleo Wazee na Watoto, na kundi la mwisho la uwezeshaji wanawake na
vijana ambalo lipo chini ya Halmashauri.
Na inaonyesha
kuwa mfuko huu wa halmashauri haukuwapa nafasi sana wanaume na kuwapendelea
zaidi wanawake kwa kuwa mwanaume anapzaliwa tayari ameshawezeshwa hivyo ana
changamoto nyingi kama mwanamke, ndio maana umri wa vijana umewekwa ni miaka
18-35 na wanawake kuanzia miaka 18 mpaka 60.
Hata hivyo
imeonekana kuwa wanawake wengi hawakaopesheki katika mabenki kwa kuwa hawana
cha kuweka rehani kama nyumba, mashamba nk. Lakini pia wanawake hao wana mzigo
mkubwa wa majukumu anapoipata fedha hiyo ambapo itatumika kwenye chakula au
shida yoyote nyumbani na matokeo yake atashindwa kurudisha marejesho ndio maana
mfuko huo umewapa nafasi kubwa wanawake hao.
Aidha muwezeshaji
huyo aliendelea kusema kuwa kituo kinakuwa na watu 50 ambao wamejigawa katika
vikundi vya watu 10 na masharti yake ni kuchukua kuanzia laki 2 au chini ya
hapo lakini ukomo wake ni milioni 5, na hii ni kwa usimamizi wa serikali za
mitaa na kata kwa kuleta taarifa sahihi za wakazi wake ili isije kutokea hali
ya sintofahamu na fedha kupotea bure.
Lakini pia
dada bertha aliendelea kusisitiza kuwa ili kuendana na sera ya serikali awamu
ya tano yakuwa na uchumi wa viwanda wao wameitumia fursa hiyo na kuongezea kuwa
ni viwanda na uchuuzi, kwani wakopaji sio wote ni wazalishaji ama wachakataji
lakini kuna madereva wa boda boda, wamachinga, wauza maji, wanawake wabeba
mabeseni nk. Hawa wote wanatakiwa kuwezeshwa na mikopo hiyo.
Na mwisho
alimalizia kwa kusema kuwa wanafanya kazi na mashirika kama SIDO, VETA, TFDA, UNIDO
nk. Kwa kuwasaidia wajasilimali wadogo wadogo wanapozalisha ama kuchakata
bidhaa zao ziwe na kiwango cha kimataifa ili kuweza kuuzika hata nje ya nchi na
hata kupata masoko katika supermarket kubwa hapa nchini.
No comments:
Post a Comment