Monday, November 20, 2017

AMANA BENKI YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA NA MIAKA 6 TANGU KUANZA KUTOA HUDUMA ZAKE

Leo ikiwa ni tarehe 20 ya mwezi wa 11 benki ya Kiislamu Amana imefanya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja na miaka sita tangu Benki hiyo ilipoanza kutoa huduma zake.
Akiongea na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Benki Dr. Muhsin Salim Masoud alisema mnamo 24/ 11/ 2011 benki hiyo ilianza kutoa huduma zake rasmi na mpaka kufikia 24 mwezi huu 2017 benki hiyo itakuwa imetimiza miaka 6 ya kutoa huduma kwa wananchi wa Tanzania.

Aidha Mkurugenzi huyo alisema kuwa Amana benki imepata mafanikio makubwa kwa hiyo miaka sita na moja ya mafanikio hayo ikiwa ni kwa mwaka jana waliweza kuanzisha utaratibu wa kutoa mikopo kwa wafanya biashara wadogo wadogo ambayo ilianzia kiwango cha milioni moja mpaka milioni kumi na imegharimu kiasi cha zaidi ya bilioni moja na nusu za kitanzania.
Lakini pia mafanikio mengine ni kuweza kupata wateja wengi waliofungua akaunti katika benki hiyo ambapo zaidi ya akaunti elfu ishirini zilifunguliwa kwa mwaka jana peke yake ambazo ni zaidi ya asilimia 25 ya akaunti zote.

Dr. Muhsin aliendelea kusema kuwa wamezindua huduma ya MasterCard ambayo imekuwa ni msaada mkubwa kwa wateja wao kwani kwa sasa wanaweza kutoa pesa katika ATM yeyote na maduka makubwa yenye huduma hiyo ndani na nje ya Tanzania.

Akiongelea mipango Mkurugenzi huyo alisema kuwa Amana kwa sasa ina matawi 7 na tawi la 8 litafunguliwa hivi karibuni mkoani Tanga, na wanajipanga kabla ya kumalizika kwa mwaka 2018 watajaribu kuhakikisha wameongeza matawi mengine mawili na kufanya jumla ya matawi kuwa 10.
Bw.Dowson Bubelwa yeye ni miongoni mwa wateja wa kwanza kabisa wa Amana Benki na yeye alisema kuwa anafurahishwa sana na huduma za benki hiyo kwani ni watu wakarimu na wenye kujali wateja wao.

Lakini pia bw. Dawson alisema alipenda kuwaambia watanzania wote wajaribu kukaribia Amana Benki kwani sio benki inayoweka matabaka kwa kuwa imeitwa benki ya Kislamu, na kusema kuwa Amana inawajari wateja wake wote hata wasio waislamu kwa kuwapa huduma sawa na wengine.

Na mwisho kabisa Bw. Dawson alisema kuwa ATM Card ya Amana imemsaidi hata alipokuwa anatibiwa nchini India aliweza kulipia huduma mbalimbali kwa kutumia Master Card hiyo ya Amana.

No comments: