Wajasiriamali
wa kote nchini wametakiwa kuwa na tabia ya kujiamini na kuwa wabunifu katika
biashara zao kwani hii ni njia pekee itakayowatofautisha wao na wafanya biashara
wengine.
Muwezeshaji Mariam Tambwe akitoa ufafanuzi wa jambo fulani, mapema jana katika Semina ya ujasiriamali iliyoandaliwa na TGNP Mtandao ofisini kwao Mabibo jijini Dar es salaam. |
Hayo
yamesemwa mapema jana na Muwezeshaji Mariam Tambwe ambaye pia ni mwalimu wa
chuo cha biashara CBE alipokuwa akiendesha semina ya namna ya kubuni biashara
kama mjasiriamali na kuifanya ikastawi na kuwa bora zaidi.
Akitoa elimu
hiyo kwa washiriki wa GDSS alisema kuwa ili uwe mjasiriamali ni lazima uwe na
vitu vikubwa vitatu vitakavyokufanya uweze kusonga mbele katika gurudumu la
maendeleo ya biashara yako ambavyo ni Elimu, Ujuzi na Hulka.
Aliendelea
kwa kusema kuwa si lazima kuwa na sifa zote tatu lakini walau uwe nazo hata
mbili ili ujiite mjasiriamali na uweze kuzimudu changamoto zinazopatikana
katika fani hiyo na si vinginevyo.
Lakini pia
alisema kuwa kunachangamoto mbalimbali zinazowakabili wajasiriamali mbalimbali
hasa wanawake, ikiwemo rushwa ya ngono kwa wateja wao au watu mbalimbali
waliowazunguka katika maeneo yao ya biashara kwa kuwataka kimapenzi ili
biashara zao ziweze kwenda vizuri.
Baadhi ya Wanaharakati wakifuatili kwa umakini Semina iliyofanyika mapema jana makao makuu ya Mtandao wa Jinsia TGNP. |
Na
changamoto nyingine ni kwa wanawake kuwa na majukumu mengi ya kifamilia yanayowakabiri
ikiwemo ulezi wa familia, kushughulikia wagonjwa na kuhakikisha watoto wanakuwa
salama katika malezi na hata kiafya bora.
Muwezeshaji
huyo aliendelea kusema kuwa changamoto nyingine kubwa ni kwa wanawake baadhi ya
maeneo hawapewi nafasi ya kumiliki ardhi wakati kwa ulimwengu wa sasa
unapohitaji mkopo wa kujiendeleza katika biashara ni lazima uwe na kitu cha
kuweka rehani ambacho ni mali isiyohamishika kama ardhi.
Aidha Dada
Mariam alisema ili uwe mjasiriamali
mzuri ni vema uwe unazaliasha ama kuagiza bidhaa nyingi isije kutokea mteja
akaja na akakosa bidhaa, kwani akikosa zaidi ya mara mbili anaacha kuja kwako
na kwenda sehemu nyingine na unakuwa umempoteza wateja.
Lakini pia
mjasiriamali anatakiwa kuwa na utofauti wa bidhaa zake na hii sio kwa kuwa na
kitu ambacho hakijawahi kutokea ama kuonekana sehemu hiyo, ila awe na kitu
chenye utofauti na ubora zaidi ya wengine.
Baadhi ya washiriki wa semina za Jinsia na Maendeleo GDSS wakimsikiliza kwa umakini Muwezeshaji wa semina hiyo Dada Mariam Tambwe akiwaelezea namna ya kufanya ili wawe Wajasiliamali kamili. |
No comments:
Post a Comment