Ndugu
waandishi wa habari: Nimeshikwa na mshtuko, simanzi baada ya kusambaa kwa taarifa ambazo naweza kusema kuwa ni za
uzushi kwamba ninampango wa kujiondoa
ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema. naomba taarifa hizo
zipuuzwe manahazina ukweli wowote na kwamba zinampango wa kunichafua mimi
pamoja na Chama Changu.
Ndugu
wandishi wa habari : Napenda ieleweke kuwa
sijawahi kudhani wala kufikiria kuhama Chadema na kwenda kwenye chama
chochote kile cha siasa. Chadema ni chama ambacho nimetoka nacho mbali tangu
mwaka 2004 hadi leo, nimejenga chama kwa gaharama zangu mwenyewe.
waandishi wa
habari: Leo nimekuwa Meya wa jiji la Dar es Salaam kupitia Chama Changu cha
Chadema,natambua kuwa chama
kimeniheshimu sana kwa kunipa nafasi hii hivyo sina sababu ya kuondoka
kwani ninania ya kuwatumikia Wananchi
ambao wameniamini na wamenichagua kwa mapenzi yao wakiamini kuwa nitawaletea
Maendeleo nikiwa ndani ya Chama Cha Chadema.
.Nafahamu tuhuma hizi zinatokana na aina ya utendaji
wangu katika Jiji la Dar es Salaam kwani nimekuwa nikifanya kazi badala ya
kupambana na serikali pale ambapo watu wanaamini kuwa mambo hayajaenda sawa.
Ndugu
waandishi wa habari: Kukaa kwangu kimya
huku ,kutokufanya siasa za kiharakati ndani ya jiji la Dar es Salaam haimanishi kwamba nipo upande wowote ama
kukihujumu chama changu. Ila huu ni mfumo ambao nimeuchagua na kujijengea kwa
ajili ya kuwatumikia wananchi nasio kufanya harakati za kisiasa kwakuwa
nina nia
ya kufanya maendeleo ndani ya jiji la Dar es Salaam.
Ndugu waandishi
wahabari: Naomba ifahamike kuwa hakuna Mkurya ambaye aliwahi kuwa
msaliti,katika nafasi yoyote ambayo aliwahi kuwa nayo. Kutokana historia hiyo,
naomba niaminike na wanachama na wananchi wote kuwa haitakuja kutokea Mkurya
mimi nikakisaliti chama changu.
Nakama itakuja kutokea nikafanya hivyo ninaweza
kuhatarisha maisha yangu, Familia yangu, na hivyo kujikuta nikaingia kwenye
matatizo makubwa ambayo kimsingi sio mazuri. Mama yangu ni mjane, kama itafanya
hivyo Chadema wote Mkoa wa Mara hawawezi kuwaacha ndugu zangu salama .
Ndugu
waandishi wa habari : Tangu nimeona watu wote waliohama ,kusaliti vyama vyao,
maisha yao yamekuwa mabaya, nahata imani kwa Wananchi wao imepungua. Hivyo na
Mimi sitaki kuwa kama wao, ninania ya
dhati ya kukitumikia chama changu kwa uaminifu mkubwa kama ambavyo wao
wameniamini.
Kuliko
kuhama Chadema ni heri mkanitafutie Mahala pengine pakuishi ambapo itakuwa ni
mbinguni lakini sio hapa duniani ama kwenda kwenye Chama kingine chochote cha kisisasa.
Kikubwa
napenda kuwaeleza wana chama wote wa Chadema kuwa hivi sasa kila mmoja tujielekeze kwa nguvu zetu zote kwenye
kampeni hivi za uchaguzi mdogo wa madiwani unaotarajiwa kufanyika Novemba 26
mwaka huu.msikubali kutolewa kwenye maandalizi ya uchaguzi.
Mwisho .
Imetolewa
leo Novemba 23/2017
Christina
Mwagala, Ofisa Habari na Msemaji Mkuu wa Mstahiki Meya wa jiji la Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment