Wednesday, November 22, 2017

KAULI YA LOWASSA BAADA YA KUONA VIJANA WANASALITI VYAMA VYAO

Waziri mkuu mstaafu wa awamu ya nne ambae pia ni mjumbe wa kamati kuu wa CHADEMA taifa Mh. Edward Lowassa amesema  kuhama kwa wanachama katika vyama vyao haiwezi kuleta tatizo kwa chama husika na watu wasichukulie kama ni jambo baya.
Image result for lowassa
Lowassa aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa jambo hilo lisiwe kigezo cha kubaguana na kuwataka wananchi kutanguliza Utanzania.
Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Tanzania alisema yeye binafsi anaamini kuwa mabadiliko ya kweli yanatoka nje ya CCM.
“Hatuwezi kugombana na kuchukiana kwasababu ya Kuhama vyama na wala tusikubali kubaguliwa hivyo, sisi ni Watanzania Kwanza. Lakini binafsi bado naamini Mabadiliko ya kweli yatatoka nje ya CCM.” aliandika Lowassa.

No comments: