Sunday, November 26, 2017

MAGARI 50 YAKAMATWA BANDARINI NA RAIS MAGUFULI, PIA ATOA KAULI KALI KWA IGP KUSHINDWA KUZUIA UFISADI ULIOPO KATIKA IDARA YAKE

Magari 50 ambayo mwenyewe hajajulikana yamekamatwa bandarini na Rais Magufuli alipofanya ziara bandarini hapo, akitokea kwenye meli ya madaktari bingwa kutoka China.
Image result for MAGUFULI BANDARINI
Magari hayo amabayo yameelezwa kuletwa mwezi wa 6 mwaka 2015 yakiwa na magari ya jeshi la polisi, mpaka leo hayajatolewa bandarini hapo, yameelezwa kuwa na siri kuba ambayo Rais mwenyewe anaifahamu, huku mzigo wa lawama ukienda kwa Jeshi la Polisi.

“Inakuwaje rais nipate taarifa za magari kufichwa lakini Waziri, TRA, TPA msijuie? Mnatakiwa muwe na informer wenu sio hadi mimi nije ndo mnaaza kusema sijui. Nafahamu hata mletaji namfahamu, nataka mniletee ninyi ili nione kama tunaenda uelekeo mmoja au hatuendi", amesema Rais Magufli.

Raius Magufuli ameendelea kwa kusema ..."Kule Polisi kuna mambo ya hovyo. Polisi Mnadai hizi gari ni zenu, kwanini hamzifuatilii tangu 2015? Kuna magari yamekaa miaka 10 lakini sheria inasema gari likikaa zaidi ya siku 21 yapigwe Mnada, kwanini hampigi mnada? IGP kwenye Majambazi upo safi lakini huku kwenye Ufisadi bado sana. Kama mtu anakunanihii mtwange. Nilikuchagua ulikua such good guy lakini unaniangusha. Polisi kuna Uchafu mwingi sana".

Kufuatia tukio hilo Rais Magufuli ametoa siku saba kwa TAKUKURU, Polisi na Wizara ya Uchukuzi kumpatia taarifa kamili juu ya magari hayio, ambayo mpaka sasa mmiliki wake hajajulikana.

No comments: