Leo ikiwa ni
tarehe 23 ya mwezi novemba benki ya Exim Tanzania imekuwa ya kwanza nchini kwa
matawi yake kupata cheti cha ISO 9001:2015 ikiwa kama uthibitisho wa ubora wa
kimataifa kutoka shirika la viwango la kimataifa.
Mkuu wa Rasilimali watu wa Exim Benki Bw.Fredreick Kanga akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mbele ya waandishi wa habari ambao hawapo pichani, mapema leo makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam |
Ikiwa ni
jukumu lao ISO kuzingatia kanuni na ubora wa viwango wa kimataifa ikiwemo
katika kujikita katika kuboresha huduma kwa wateja, kuangalia hamasa na msukumo
wa viongozi wa juu mashirika, michakato na oparesheni zinavyoendeshwa, Exim
benki imeonekana kuwa na vigezo hivyo na kutunukiwa cheti na ISO.
Akiongea na
waandishi wa habari katika hafla ya kupokea cheti hicho Mkuu wa Rasilimali watu
Bwa. Fredreik kanga alisema uthibitisho huo ni miongoni mwa mafanikio makubwa
ambayo benki hiyo imepata ikiwa ni pamoja na benki kupata tuzo hivi karibuni
kutoka banker – Afrika Mashariki kuwa benki bora kwa wateja binafsi.
“Kupata
uthibitisho huu kutoka ISO ni hatua muhimu katika kuonyesha msimamo wetu wa
kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wetu, lengo letu ni kuendelea kuboresha
imani katika soko kwa wateja wetu, kuboresha utoaji huduma, kupunguza muda wa
kutoa huduma, kuwa tofauti na benki zingine, kuongeza ufanisi na pia kupata
faida na kuongeza soko letu” alisema Frederick Kanga
Mradi huo
ulichukua takribani miezi 6, ulianza kwa kutoa mafunzo kwa wafanyakazi juu ya
kanuni za usimamizi wa ubora wa kimataifa ISO 2001:2015, pia uboreshwaji wa
viwango, ukaguzi wa ndani utengenezaji wa ratiba ya matukio kuwekamipango
muhimu hadi kufikia upatikanaji wa uthibitisho huo na ilikuwa kujitoa kwao na
utendaji bora ambao umesababisha tuzo hii.
Katika
kuhakikisha inajenga chapa bora benki ya Exim imejikita katika kuhakikisha
inakuwa na bidhaa za kivumbuzi , mahusiano bora na kutoa huduma kwa haraka, na
ikumbukwe kuwa mchakato huu wa kupata cheti cha ISO ulianza mwaka huu na Clock
Tower na Namanga yaliteuliwa kuwa ya kwanza kupatiwa mchakato huo.
Mkuu wa
rasilimali watu wa Exim aliendelea kwa kusema “Tukiwa kama benki yenye
uthibitisho wa ISO tutahakikisha utoaji wa huduma na bidhaa ni bora, ufanisi
katika operesheni na mawasiliano, hamasa kwa wafanya kazi na ongezeko la mauzo
na masoko”.
Kwa upande
wake mwakilishi wa ISO Bw. Nyasha Mupukuta alisema kuwa shirika hilo
lilianzishwa kwa dhumuni la kujibu swali la “je ipi ni njia bora zaidi ya
kufanya jambo?”
“ISO
imetengeneza viwango vinavyozingatia kila sekta hivyo basi kampuni inayopata
kuthibitishwa na ISO ina maana kuwa watumiaji wanaweza kuwa na uhakika kwamba
bidhaa wanazozitumia ni salama za kuaminika na za ubora wa hali ya juu”.
aliongezea Nyasha Mupukuta
No comments:
Post a Comment