Monday, November 13, 2017

SHIRIKA LA MOTHERS HELPING MOTHERS WAJIPANGA KUCHANGIA DAMU KUSAIDIA WANAWAKE WAJAWAZITO

TaasisI inayojihusisha na kusaidia wamama wanaolea watoto bila msaada wa baba zao, wanawake wanaotumia madawa ya kulevya na kusaidia wamama wajawazito na ujasiriamali ya Mothers helping Mother wameshiriki shugguli za usafi katika hospitali ya mwanyamala mwishoni mwa wiki ikiwa ni moja ya njia ya kuhamasisha jamii kufanya kazi ya kumkomboa mwanamke pamoja na kuondokana na dhana potofu ya kuamini kuwa wanawake hawawezi kufanya jambo.
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu Mratibu wa shirika hilo Haiba Msafiri ,amesema kuwa wao kama shirika linalolenga kumsaidia mwanamke wameamua kwa moyo mmoja kumsaidia mwanamke kutoka katika uonevu katika jamii.huku wakiitaka jamii kuwaunga mkono katika juhudi hizo

Shirika hilo la Mothers helping mothers watakuwa na zoezi la kuchangia damu kwa ajili ya wamama wajawazito trh 18/11 zoezi litakalifanyika eneo la msimbaz center
Kwa taarifa zaidi kuhusu shirika hilo unaweza kuwafuatilia kupitia mitandao ya kijamii kwa  page yao insta ya mothers_helping_mothers

No comments: