Serikali imeokoa
kiasi cha Shilingi Bilioni 24,556,724,598 na Dola za Marekani 7,817,170.48 kupitia mashauri ya madai ambayo
Serikali ilishinda yaliyoendeshwa katika mahakama mbalimbali nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Mdemu alipokuwa akiwasilisha
taarifa ya utekelezaji ya ofisi yake kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa
fedha 2017/18 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipokutana
mjini Dodoma.
Amesema wameiwezesha Serikali Kushinda kesi kwenye mashauri 23 yaliyokuwa
yanahusisha madai ya fedha na kuongeza kuwa kama Serikali isingekuwa makini na
kushindwa kesi ingelipa kiasi cha shilingi 24,556,724,598 na na Dola za
Marekani 7,817,170.48.
“Kama Serikali isingekuwa makini na kushindwa kesi ingelipa
kiasi cha shilingi 24,556,724,594 “Hivyo basi kwa kushinda kesi hizo, Serikali
imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi 24,315, 498,042.44 na Dola za Marekani 7,817,170.48 na hivyo kupoteza kiasi cha
shilingi 241,226,557.56, kwa kesi ilizoshindwa”, alifafanua.
Amesema ofisi yake imeendelea kutekeleza kikamilifu jukumu
lake la kutoa ushauri wa kisheria kwa serikali na Taasisi zake na na kuwezesha
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile mradi ya bomba la
mafuta kutoka Hoima hadi Tanga ambayo italeta ajira na kuchangia mapato kwa
Serikali.
Amesema Ofisi yake pia imeendesha mashauri 169 ya kikatiba
yakiwemo mashauri mapya 37 , mashauri hayo yote yapo katika hatua mbalimbali
ambapo Mashauri 25 yalihitimishwa na kufanya kubaki mashauri 144 ambayo
yanaendelea kufanyiwa kazi .
No comments:
Post a Comment